Habari za Punde

*WAKAZI WA ZANZIBAR WAPIGA KURA YA MAONI KWA AMANI


Dk. Gharib Bilali, akizungumza na waandishi wa habari bada ya kumaliza kupiga kura ya maoni katika Kituo cha Kiembe Samaki mjini Zanzibar leo.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo, akionyesha karatasi ya kura yake ya NDIYO baada ya kupiga kura katika Kituo cha kupigia kura ya Maoni cha Migombani mjini Zanzibar
Mwandishi wa habari wa Televisheni ya Chanel Ten Munir akipiga kura ya Maoni.

Baadhi ya Vituo vilikuwa tupu havina watu kama Kituo hiki cha Bwawani kikiwa hakina watu.

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, akipiga kura ya maoni katika Kituo cha Shule ya Msingi Mtopepo Mtoni mjini Zanzibar leo asubuhi. Katika Kituo hicho wamejitokeza watu wengi kupiga kura hiyo tofauti na vituo vingine vya mjini Zanzibar, ambapo vituo vingi wamekuwa wakijitokeza wananchi mmoja mmoja na kupiga kura na kisha kuondoaka kwa usalama tofauti na ilivyotarajiwa na wengi kwamba huenda ingezuka vurugu kutokana na baadhi ya watu kuipinga hoja hiyo ya kura ya maoni ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Ama kwa hakika Wakazi wa Visiwa vya Zanzibar wameitikia wito na kuipokea kwa mikoni miwili hoja hiyo n kuifanyika kazi ili kuweza kuleta mabadiliko visiwani humo.

Wakazi wa Migombani mjini Zanzibar wakiingia kwenye kituo hicho na wengine wakitafuta majina yao kwenye ubao wa matangazo kabla ya kuingia kwenye vyumba vya kupigia kura leo mchana.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.