Habari za Punde

DK. BILAL AFUTA YA PROF. LIPUMBA MAFIA

Mgombea Mwenza wa Urais kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akiagana na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mafia, Abdulkarim Shah, mara baada ya kumaliza mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Kilindoni Wilaya ya Mafia Mkoa wa Pwani leo jioni, ikiwa ni pamoja na kumnadi mgombea huyo na Madiwani wa Kata za kisiwa hicho.
Katibu Mwenezi Mstaafu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Haji Manara akizungumza jukwaani ikiwa ni sehemu ya utangulizi kabla ya kupanda Mgombea Mwenza Dk Bilal wakati wa mkutano huo wa kampeni.

Wananchi Wilaya ya Mafia eneo la Kilindoni Mkoa wa Pwani wakimsikiliza na kumshangilia Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Visiwani humo leo joni.

Green Guard wa Mafia wakimvisha Skafu Mgombea Mwenza Dk Bilal, baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Wilaya hiyo leo.




No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.