Habari za Punde

*airtel TANZANIA YAWASHUKURU WADAU NA WATEJA WAKE KUELEKEA MWAKA MPYA

Ndugu zangu wapendwa, Heri ya sikuku na pia napenda kuchukua nafasi hii ya pekee kuwatakia wote heri ya sikuku na kuwashukuru kwa ushirikiano wenu katika kipindi hiki cha mwaka 2010. Nina imani kabisa mafanikio ya Airtel yameletwa na ushirikiano wenu,msaada pale tulipohitaji kuwafikia watanzania na vile vile moyo wenu wa kusaidia, napenda kuwatumia maazimio yetu ya kipindi cha 2011, Nawatakia kila la Kheri, Wenu katika ujenzi wa Taifa Beatrice Singano Mallya

Disemba 31, 2010

FOR IMMEDIATE RELEASE

Airtel yajizatiti kuongeza ufanisi kwa wateja wake Afrika 2011

· Wateja kupata mawasiliano ya kiwango cha juu ya uhakika na teknolojia mpya popote walipo

· Kuwekeza katika jamii na kuwezesha shule Afrika

Nairobi, Kenya Bharti airtel – kampuni ya simu za mkononi ya tano kwa ukubwa duniani – imedhamiria kuimarisha mtandao wake Afrika mwaka huu.

Manoj Kohli,Ofisa Mtendaji mkuu wa Kimaitaifa wa Aitel - CEO (International) na Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Afrika, alisema: "napenda kuchukua nafasi hii kuwatakia wateja wetu na washikika wetu wote tunapoanza mwaka mpya.Tutaendelea kwapatia huduma zilizobora na za uhakika na kuhakikisha tunapeleka huduma zetu kwenye pembe zote vikiwemo miji na vitongoji vyake,kwa kupitia mawasilaiano ya 3G katika bara la Afrika; nia na madhumuni yetu ni kuhakiksha wateja wetu wanapata mawasiliano bora na kuendelea kuchagua na kutumia huduma zetu.”

Mr. Kohli aliongeza, “Tunazishukuru serikali kwa kutupatia msaada wa dhati.Tunataka kuwa wabia katika kukua kwa bara la Afrika kwa kufanya kazi na serikali na mamlaka za mawasiliano kuwezesha ukuaji wa mawasiliano katika sehemu zote za jamii.”

Ahadi ya unafuu wa bei za mawasiliano na teknolojia ya kisasa

Katika harakati itakayoIeta mabadiliko na ukuaji wa mawasiliano ya simu za mkononi Afrika na kuleta maendeleo mazuri ya kasi katika bara la Afrika , Bharti Airtel Limited na IBM tulitangaza uchaguzi wa IBM kuangalia na kusimamia maswala ya teknolojia ya komputa na huduma zitakazo ongeza ufanisi wa huduma za simu za mkononi zinazotolewa na mtandao wa Bharti Airtel.

IBM italeta teknolojia mpya Afrika kutoka katika kitengo cha utafiti cha IBM , pia itajumuisha “Spoken Web” – sauti inayowezeshwa kwenye Internet ambayo inawapa nafasi watumiaji wa mtandao wa intaneti kwa pamoja kuwasiliana na kupeana habari kwa kuongea katika mtandao wa simu walio nao, ambayo ni rahisi kwa watu wasio na elimu ya kiwango cha juu cha kutumia intanet,matatizo ya kuona na mawasiliano ya Kompyuta.

Kwa kuongezea, IBM ina mpango wa kuanzisha ujanzo wa vionjo vya muziki na video , na vile vile kusaidia wanaotengeneza vionjo hivi Afika kama muziki na filamu ambao kwa sasa unakua kwa kasi.

Vile katika ushiriki wetu na makampuni kama Ericsson, Huawei na NSN kutaendelea kuimarisha ubora wa mtandao wetu Afrika na kusambaza mtandao wa 2G na 3G kuyafikia maeneo mengi zaidi. Kwa kuangalia mabadiliko ya Dunia, Afrika bado inahitakji mawasiliano ya intanent na vionjo vyake zaidi.Utumiaji wa teknolojia mpya hizi utaiwezesha Airtel kutoa nafasi na kutoa huduma za kusisimua katika mwaka wa 2011.

Mr. Kohli alieleza : “Ubia unatupeleka katika hatua moja zaidi ya mtizamo wetu wa kutoa huduma zinazopatikana kote kwa bei nafuu na kwa kila mtu Afrika , hata kule kwenyye maeneo ya pembezoni kabisa ambako hakuna mawasiliano kwa sasa.Vile vile tunajenga msingi wa kuleta mawasiliano ya 3G HSPA kama mawasiliano yanayo weza kutumika na kila mtu Afrika. Mobile broadband ni kiungo cha kuleta maendeleo ya kiuchumi.Wengi wa wateja wetu watapata mawasiliano ya Intaneti kwa mara ya kwanza katika maisha yao.”

Chaguo la IBM, Tech Mahindra na Spanco ni wabia wa mkakati wa kibiashara katika kufanya kazi kwa kushirikiana “Business Processing Outsourcing (BPO)” mpango huu utawapatia wateja wetu wa Airtel mtandao wa kimataifa na kutumia huduma zilizopo. Faida nyongeza ya mpango huu itakua upatikanaji wa ajira nyingi zaidi katika nchi zote Airtel inakotoa huduma zake Afrika.Washirika wetu wa kimataifa pia watajenga ufanisi wa kazi na uwezo kwa rasili mali watu watakaowatumia.

Jitihada hizi ,ni ongezo kwa huduma tunazotoa kwa sasa kama -( airtel Money)huduma ya Airtel ya kutuma na kupokea pesa – ambayo inaashiria makusudio endelevu ya airtel kutoa huduma bora kwa jamii.

Kusaidia Jamii

Kwa kutambua umuhimu wa elimu kama msingi imara wa mototo na kizingiti kikubwa cha kuondoa umasikini , airtel inadhamira ya kuwafikia na kuwainua wale wote wasio na uwezo wa kupata elimu bora kwa kuwekeza katika elimu.

Mpango wa shule zinazoangaliwa na Airtel (Airtel Shule Yetu ) ulizinduliwa rasmi mwaka 2010,kwa kushirikiana na serikali tunafanya ukarabati wa shule, kutoa unifomu,vitabu na madaftari,madawati, vifaa vya kufundishia na mtandao wa intaneti kwa shule hitaji.Mpaka leo watoto , 9,000 wanaohitaji msaada wa elimu wamesha saidiwa katika shule za nchi 14 kupitia mpango huu.

Katika mwaka 2011, airtel itaendelea kuimarisha na kuendeleza elimu katika nchi 16 barani Afrika.

About airtel in Africa

airtel is the new brand name for the 16 Zain operations across Africa which were acquired by airtel International in June 2010. airtel is driven by the vision of providing affordable and innovative mobile services to all. airtel has African operations in: Burkina Faso, Chad, Democratic Republic of the Congo, Republic of the Congo, Gabon, Ghana, Kenya, Malawi, Madagascar, Niger, Nigeria, Seychelles, Sierra Leone, Tanzania, Uganda and Zambia. airtel International is a Bharti airtel company. For more information, please visit www.airtel.com

About Bharti airtel Limited

Bharti airtel Limited is a leading global telecommunications company with operations in 19 countries across Asia and Africa. The company offers mobile voice & data services, fixed line, high speed broadband, IPTV, DTH, turnkey telecom solutions for enterprises and national & international long distance services to carriers. Bharti airtel has been ranked among the six best performing technology companies in the world by BusinessWeek. Bharti airtel had over 202 million customers across its operations at the end of November 2010. To know more visit www.airtel.in


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.