Habari za Punde

*BENKI YA KCB YATIMIZA AHADI YA SH. MILIONI 10 KWA LYASIKIKA SEKONDARI WILAYANI HAI

Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB Tanzania, Dk. Edmund Mndolwa (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya Sh. Milioni 10, Mkuu wa Wialaya ya Hai, Norman Adamson, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi ya benki hiyo kwa ajili ya ujenzi wa Darasa la Shule ya Sekondari ya Lyasikika iliyopo Wilayani Hai Mkoa wa Kilimanjaro, hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo, Christina Manyenye na Mkuu wa Mikopo wa benki hiyo, Ronald Kitti.
Mkuu wa Wilaya ya Hai, Norman Adamson, akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya Sh. Milioni 10, kwa (katikati) kwa ajili ya ujenzi wa Darasa la Shule ya Sekondari ya Lyasikika iliyopo Wilayani Hai Mkoa wa Kilimanjaro, iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB Tanzania, Edmund Mndolwa, (kushoto) ni Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo, Christina Manyenye.
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB Tanzania, Edmund Mndolwa, akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya Sh. Milioni 10, kwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Norman Adamson (katikati) kwa ajili ya ujenzi wa Darasa la Shule ya Sekondari ya Lyasikika iliyopo Wilayani Hai Mkoa wa Kilimanjaro, iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo, Christina Manyenye.


















No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.