Habari za Punde

*MAKHIRIKHIRI, RUFITA WAFANYA MAKAMUZI BALAA MKESHA WA KRISMAS

Wasanii wa kundi la Makhirikhiri kutoka nchini Botswan, wakila pozi wakati wakiwajibika jukwaani kwenye onyesho la pamoja na bendi ya Rufita Connection, iliyo chini ya Banza Stone kwenye Ukumbi wa Msasani Beach Club Dar es Salaam, wakati wa Mkesha wa Sikukuu ya Krismas usiku wa kuamkia leo.
Shabiki wa miondoko ya kundi hilo, aliyepagawa vilivyo na miondoko hiyo, akionyesha umahiri wake wa kusakata midundo ya Makhirikhiri jukwaani wakati kundi hilo likiendlea kuwapagawisha mashabiki lukuki waliohudhuria onyesho hilo.
Shabiki wa kundi hilo, aliyejulikana kwa jina moja la Lucy, akiwatunza wasanii wa kundi hilo jukwaani.
Mashabiki wa kundi hilo, wakipiga picha ya kumbukumbu na mmoja wa wanenguaji wa kundi hilo (wapili kushoto).
Kiongozi wa bendi ya Rufita Connection, Banza Stone (katikati) akiwa na baadhi ya wanamuziki wa bendi yake wakati wa onyesho hilo.
Kila mbongo aliyekuwamo ukumbini humo alitamani kupiga picha ya kumbukumbu na wasanii hao, hapa ni shabiki akipiga picha ya kumbukumbu na mmoja kati ya wasanii wa kundi hilo.
Wakazi wa jijini Dar es Salaam, wakisebeneka na miondoko ya Makhirikhiri.
Kila mmoja yuko bize na miondoko hiyo.
Wasanii wa kundi hilo wakishambulia jukwaa.
Makamuzi yanaendelea jukwaani.
Si unacheki mwanaume yupo kazini hapa....











No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.