AJALI mbaya ya ndege ndogo iliyotokea jana mkoani Mbeya imeua mwanafunzi mmoja wa Shule ya Sekondari Swilla, iliyopo mji mdogo wa Mbalizi Wilaya ya Mbeya Vijijini, Godfrey Mpolia, mbaye amefariki papo hapo na wengine watatu kujeruhiwa baada ya ndege hiyo waliyokuwa wakisafiria kutoka Mbeya kwenda Dar Es Salaam kuanguka.Ndege hiyo inayomilikiwa na kampuni ya Tropical-Air Z yenye namba SH-PCN U206F imeanguka majira ya saa 6;39 katika eneo la Uyole nje kidogo na jiji la Mbeya muda mfupi baada ya kuondoka katika uwanja wa ndege mkoani humo kuelekea jijini Dar es salaam.
Nege hiyo ilikodiwa na Mfuko wa Bima ya Afya kwa ajili ya kuja Mbeya kumchukua mwanafunzi huyo aliyemaliza kidato cha Nne mwaka huu, ambaye ni marehemu aliyefariki katika ajali hiyo, aliyekuwa mgonjwa kwa ajili ya kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Muuguzi wa zamu wa Hospitali ya Rufaa Mbeya,Suma Kibopile, akizungumza na SUFIANIMAFOTO kwa njia ya simu, alisema wamepokea majeruhi watatu ambao ni pamoja na Dakrati wa Rufaa kitengo cha Mifupa, Dk.Jons Chitemo, ambaye alikuwa akimsindikiza mwanafunzi huyo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Kibopile alisema majeruhi wengine wa ajali hiyo ni Rubani wa ndege hiyo,Keyuln Fakhard raia wa Iran ambaye amelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya kutokana na kupata mshituko baada ya kupata taarifa kuwa mwanafunzi aliyekuja kumchukua amefariki dunia na Muuguzi Frorence Stephen ambaye hata hivyo ametibiwa na kuruhusiwa.
Balama alisema ajali ya ndege iliyotokea jana nayo imekuwa siku chache tu baada ya kuungua kMkuu wa Wilaya ya Mbeya, Venance Balama, ambaye alifiki eneo la tukio amesema kuwa ajali hiyo imeleta historia nyingine kwani mwaka 2006 kulitokea ajali ya ndege katika uwanja huo ambapo Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Bunge, Juma Akukweti alipata ajali na kufariki wakati ametoka kuangalia soko la Mwanjelwa lililoungua mwaka huo.

No comments:
Post a Comment