Habari za Punde

*NGELEJA-SASA TATIZO LA MGAO WA UMEME KUMALIZIKA JUMAMOSI

Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja (kuliao) akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Mtambo wa Songas, Robert Kofsky, wakati akimtembeza kukagua mitambo ya Songas na mtambo namba 4 wa LPT uliofanyiwa ukarabati kwa ajili ya kufungwa katika mtambo ulioharibika hivi karibuni na kusababisha matatizo ya mgao wa umeme. Ngeleja alifanya ziara katika vituo vya kuzalisha umeme vya Songas, IPTL na mtambo wa Umeme wa Tegeta nakujiionea Mtambo huo ambao ni miongoni mwa mitambo iliyosababisha tatizo hilo, ambapo inatarajia kukamilika Jumamosi wiki hii baada ya kufungwa na kumaliza kabisa tatizo la mgao wa umeme.

Ngeleja ageuka 'Trafic kwa muda' Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, akisimamisha magari ili kuvusha waandishi wa habari pamoja naye, wakati walipokuwakatika ziara hiyo ya kutembelea mitambo ya kuzalisha uememe leo mchana
Ngeleja akizungumza na waandihi wa habari baada ya kumalizika kwa ziara hiyo.



No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.