Habari za Punde

*ASKARI WATOA MAFUNZO YA USALAMA BARABARANI KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI LEO

Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Mafunzo ya Usalama barabarani, Inspekta Abel Swai, akiwaelekeza jambo baadhi ya wanafunzi wa Shule za Msingi za Oysterbay, Kumbukumbu na Mbuyuni, wakati wa mafunzo maalum ya kuwafundisha kuvuka barabara kwa kutumia alama za usalama Barabarani, yaliyofanyika kwenye Barabara ya Ali Hassan Mwinyi Dar es Salaam leo mchana.
Mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi, Mbuyuni jijini Dar es Salaam, akisimamisha magari kwa kutumia kifaa maalum kwa ajili ya kuwavusha baadhi ya wanafunzi wenzake baada ya kupata Elimu ya Mafunzo ya Usalama Barabarani na kutumia vifaa vya alama za Barabarani yaliyofanyika jana na kuwashirikisha wanafunzi wa Shule za Msingi za Oysterbay, Kumbukumbu na Mbuyuni.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.