Habari za Punde

*CHEKA AMALIZA UBISHI WA MPINZANI WAKE MAUGO

Bondia Mada Maugo, akiingia jukwaani kwa staili yake ya kupita juu ya kamba za ulingo, ambapo kabla ya kulingia kila mmoja alikuwa akimtegea mwenzake aanze kuingia.
Cheka naye akiingia jukwaani baada ya mpinzania wake kuingia.Sasa Mtanange huo wa kuchakazana unaanza.....kila mmoja yupo kwenye kona yake.
Bondia Mada Maugo (kulia) arusha konde zito kwa mpinzani wake, Francis Cheka wakati wa mpambano huo.
Bado Mada maugo (kulia) anaendelea na kasi ya kujaribu kumuwahi mpinzani wake Francis Cheka.
Mashabiki lukuki waliojitokeza kushuhudia mpambano huo uliokuwa ni wa upinzani zaidi kutokana na jinsi mambondia hao walivyokutwa wamekaniana, hadi kutaka kuzichapa kavu kavu siku walipokuwa wakipima uzito huku kila mmoja akionyesha hasira zake kwa mwenzake.
Maugo alianza kupungua kasi yake aliyoingia nayo katika raundi ya tano ambapo Cheka alikuwa akimwelemea muda wote, hapa Maugo akikwepa konde zito la Cheka.
Bado wanaume wanaonyeshana ubavu kwa kurushiana makonde.
Baada ya mchezo huo kumalizika Cheka alitangazwa mshindi kwa kumzidi mpinzani wake kwa pointi, hapa ni mashabiki wake wakimbeba na kushangilia naye baada ya ushindi huo.
Mashabiki wakiendelea kushangilia ushindi huo.
"WE KIJANA ANGALIA NISIKUPE YA UKWELI OHOOO!, ZAMANI NILIKUWA BONDIA MIMI"
Kamanda Kova (kushoto) akizindua pambano hilo kwa kuigiza kucheza masumbwi na mmoja kati ya waandaaji.
Kamanda Kova, aliyekuwa mgeni rasmi katika pambano hilo (katikati) akiwa na Makamanda wa Kanda Maalum wa Temeke na Kinondoni ukumbini humo.
Mashabiki wa ngumi wakihamaki ukumbini humo wakati mapambano ya utangulizi yakiendelea baada ya mmoja wa wapigapicha wa Televisheni kupanda jukwaani ili kupata picha bomba jambo ambalo liliwaudhi mashabiki hao na kuanza kupiga kelele na kutaka kumshusha kwa nguvu kwa kile walichodai alikuwa akiwakinga.

MAPAMBANO YA UTANGULIZI
Mabondia waliocheza mapambano ya utangulizi, Ramadhan Mashudu (kushoto) na Albet Mbena, wakichapana katika pambano lao la utangulizi la raundi sita. Katika pambano hilo, Mashudu alishinda kwa Pointi.
Mabondia Cosmas Cheka (kulia) na Husein Mbonde wakichuana jukwaani katika pambano la raundi 6. Katika pambano hilo Mbonde alishinda kwa Pointi.














No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.