Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, wakati akizungumzia na kulaani vitendo vya Askari vya kuwapiga na kuwajeruhi wananchi wanachama wa CHADEMA waliokuwa wakiandamana Jijini Arusha jana kwa kile walichokuwa wakidai kuwa ni haki yao ya msingi kufanya maandamano hayo kwa kulaani matokeo yaliyokuwa yametolewa awali kuhusu mgombea wa chama hicho katika nafasi ya Umeya kuwa 'amechakachuliwa', Lipumba amewaunga mkono CHADEMA na kudai kuwa polisi hawakutenda haki kuwasambaratisha kwa mabomu na risasi za moto kiasi cha kusababisha vurugu. Katika vurugu hizo watu watatu wamedaiwa kufa na wenginge sita kujeruhiwa. Kulia ni Kaimu Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara, Julius Mtatiro.
NMB yazindua Worldwide Pesa, Hakuna Mipaka kutuma fedha EAC, SADC
-
NA MWANDISHI WETU
BENKI ya NMB imezindua Huduma ya Kimkakati kwa Ustawi wa Sekta ya Fedha na
Uchumi wa Taifa ‘NMB Worldwide Pesa, inayowapa fursa Watanzan...
1 hour ago
No comments:
Post a Comment