Habari za Punde

*SERIKALI YAINGILIA KATI VURUGU ZA KISIASA ARUSHA

Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha, akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa tamko kuhusu vurugu za CHADEMA zilizorindima mkoani Arusha jana. Kushoto ni Inspekta Jenerali wa Polisi, Saidi Mwema. Picha kwa hisani ya Michuzi


SERIKALI imezitaka pande zinazotofautiana Kisiasa Mkoani Arusha, kukaa chini na kuzungumza na kutafuta ili kuweza kumaliza tofauti zao na kuwa kitu kimoja ili kuepuka Vurugu za mara kwa mara.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mchana, Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha, akiwa na Inspketa Jenerali wa Polisi Saidi Mwema, ikiwa ni siku moja tu baada ya kutokea vurugu baina ya polisi na wafuasi wa CHADEMA wakati wanachama hao wakifanya maandamano yanayodaiwa kutokuwa ya halali.

Ambapo katika maandamano hayo watu watatu wamepoteza maisha na wengine sita kujeruhiwa.

Nahodha, alisema Serikali imeamua kuingilia kati mgogoro huo kwa kuziweka meza moja pande mbili zinazokinzana ili kuleta amani upya jijini Arusha.

Aidha Nahodha amesema askari polisi yeyote ambaye itathibitika alikwenda kinyume na sheria ya kazi atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Viongozi wa CHADEMA na wafuasi wao waliandamana jana jijini Arusha wakielekea uwanja wa NMC ambako walikuwa wana mkutano wa hadhara. IGP Mwema alikuwa ameshatoa tangazo jana yake (juzi) kwamba maandamano yamezuiwa na yakifanyika ni batili.

Juhudi za kumpata tena Mh. Nahodha kwa ufafanuzi zinaendelea, kwani kuna shauku ya kujua kwamba baada ya serikali kuingilia kati mgogoro huo unaotokana na sakata la uchaguzi wa Meya wa Arusha uliokwamba, je wana CHADEMA waliosomewa mashitaka leo watafutiwa kesi zao?




No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.