Rais wa Kampuni ya RPB, Rahma Al Kharoous, akizungumza na waandihi wa habari baada ya kumalizika kwa mchezo wa kirafiki katika ya Yanga na Atletico ya Brazir uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa leo jioni.
Na Sufianimafoto Reporter, jijini
KUTOKANA na muitikio mdogo wa mashabiki wa soka waliojitokeza kushuhudia mchezo wakirafiki baina ya Yanga ya Dar es Salaam na Atletico Paranaense ya Brazir kwenye Uwanja wa Taifa leom, Rais wa Kampuni ya RPB Oil, Rahma Al Kharoous, amesema kuwa mchezo wa keshokutwa kati ya Simba na timu hiyo kiingilio itakuwa ni bure.

Akizungumza na Waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Rahma, ambaye ndiye mratibu wa michezo hiyo ya kirafiki, alisema kuwa ameamua kufanya kiingilio kuwa bure ili mashabiki wengi waweze kujitokeza kushuhudia mchezo huo na kuishangilia timu ya Simba ili kuwapa morari waweze kushinda.
Aidha alisema kuwa iwapo Simba itaweza kuibuka na ushindi basi ataigharamia timu hiyo ya Simba kuisafirisha hadi nchini Brazir kwa ajili ya mchezo wa marudiano na kuwataka mashabiki wengi kujitokeza kushuhudia mchezo huo.
No comments:
Post a Comment