NCHI ya Misri imesema inaandaa mikakati ya kuanzisha Shirikisho la Soka kwa Nchi za Bonde la Mto Nile., ambapo hivi sasa imeanza mazungumzo na nchi ambazo zipo katika Bonde la Mto Nile, ili kuzishawishi ziweze kukubali kuanzishwa kwa shirikisho hilo ambalo Misri inaamini litakuwa ni kitovu cha vipaji vya soka Afrika.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Rais wa Chama cha Soka cha Misri (EFA), Samir Zahir, alisema iwapo nchi zote zitakubaliana ushawishi huo wa kuanzisha shirikisho hilo, itakuwa ni hatuoa kubwa ya mafanikio na maendeleo ya Soka la Afrika.
Hata hivyo EFA, bado inaona ugumu juu ya kuanzishwa kwa shirikisho hilo kwa vile baadhi ya nchi tayari zipo katika vyama mbambalimbai vinavyosimamia soka kwa kanda zao.
Alisema zaidi ya nusu ya nchi zinazoshiriki mashindano hayo ya Bonde la Mto Nile yaliyoanza jana jijini hapa ni wanachama wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), ukiacha Misri na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ambayo ni mwalikwa katika michuano hiyo.
Nchi zinashiriki michuano hiyo ambazo ni wanachama wa CECAFA ni Tanzania, Kenya, Uganda, Sudani na Burundi na zimekuwa zikishiriki mashindano yanayoandaliwa na baraza hilo karibu kila mwaka.
"Tumepeana changamoto ya namna bora ya kuanzisha shirikisho letu, uwezo wa kufanya hivyo tunao maana dhamira yetu ni kuendeleza soka," alisema.
Nchi nyingine wanachama wa CECAFA ambazo hazijashiriki michuano ya Mto Nile ni Ethiopia, Eritrea, Djbouti, Rwanda na Somalia.
Misri imegharamia usafiri wa kuja Misri na kurudi nyumbani kwa kila timu pamoja na posho za wachezaji na waamuzi, zawadi mbalimbali kwa washindi.Bingwa wa michuano hiyo atazawadiwa zaidi ya sh. milioni 200 za Tanzania.
Bingwa wa michuano ya Chalenji inayoandaliwa na CECAFA na kushirikisha nchi 12 alizawadiwa dola za Marekani 30,000 ambazo ni karibu sh. milioni 43 za Tanzania.
Wakati huohuo, Rais huyo wa EFA, alieleza kuwa michuano yao ni maalum kuhamasisha soka na haihusiani na masuala ya kisiasa na kwamba mambo yanayohusiana na siasa ni jukumu la wahusika wenyewe.
"Kwangu mimi ukiniuliza michuano ya soka kwa nchi za Bonde la Mto Nile ina madhumuni gani, nitakwambia ni kuinua soka. Hilo ndilo jibu langu na ndicho ninachokiamini," alisema.
Alieleza kuwa mwaka huu mashindano hayo yamefanyika Misri, hivyo nafasi ipo wazi kwa nchi nyingine ambayo itakuwa tayari kuyaandaa na kamba Misri itatoa msaada wa karibu zaidi ili kuyafanikisha.

No comments:
Post a Comment