MKAZI wa Butu Ugweni Wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro Idrisa Salum (56) anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa tuhuma za kuua mtoto wake, Kibwe Idrisa (15) baada ya kumtuhumu kuiba fedha shilingi elfu 35 mali ya kaka yake.
Habari zilizotolewa na Kaimu kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Yusuph Ilembo, zimesema kuwa Kibwe aliuawa na baba yake Januari 4 mwaka huu, majira ya saa 8 mchana nyumbani kwao kwa kumpiga na fimbo pamoja na ubapa wa panga
Aidha imedaiwa kuwa baba huyo alichukua hatua hiyo ya kumuadhibu Kibwe, baada ya kutuhumiwa kuiba fedha za kaka yake Daudi Idrisa (25) jumla ya Sh. elfu 35.
Alisema kuwa baba huyo aliamua mtoto wake kumchapa ili aweze kusema alikopeleka pesa hizo za kaka yake lakini kabala ya kusema ziliko mtoto huyo alipoteza fahamu na hatimaye kufariki muda mfupi wakati akipelekwa hospitali .
Kutokana na tukio hilo Kaimu kamanda huyo amewaka wananchi kuacha kuchukua hatua za haraka kabla ya kufikiria madhara yatakayotokana adhabu wanayoitoa kwa watoto wao.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Usangi Wilayani Mwanga kwa ajili ya uchunguzi zaidi ingawa upelelezi juu ya tukio hilo bado unaendelea
No comments:
Post a Comment