Akizungumza na Sufianimafoto, Mumewe huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema kuwa ameamua kumsindikiza na kuwaomba wahusika ili kupatiwa mahala pa kulala na mkewe huyo ikiwa ni moja ya kumlina mkewe na kudumisha mila za kwao.
Mumewe huyo aliyeongozana na Kaka wa mshiriki huyo, muda wote walionekana kambini hapo wakiwa na vijifurushi vyao wakiwa nje ya Hoteli hiyo waliyofikia warembo hao wakisubiri muafaka.
Kana kwamba hawakujua kinachoendelea kuhusu mashindano hayo na taratibu zake, mume huyo na Kaka wa mshiriki huyo, walithibitisha hayo wakati wakihojiwa na Sufianimafoto, pamoja na waandishi waliohudhulia uzinduzi wa kambi hiyo leo.
Bila wasiwasi wakizungumza kiswahili kwa taabu, angalau kuliko hata huyo mrembo mwenyewe, walisema kuwa, wamefika mahala hapo kumsindikiza mshiriki huyo, ambaye kamwe hawaamini kumuacha pekee.
Naye mrembo huyo akionyesha ishara ya upole uliopitiliza wakati akihojiwa na kujibu kwa kilugha huku akifinyafinya kucha zake, alisema kuwa, amefika mahala hapo kushiriki shindano la JITAMBUE KISURA, lakini hakuzoea kuwa mahala bila mumewe na ndiyo maana wameamua kusindikizana. Sasa kama mambo yenyewe ndo kama hivi kunakujitambua kweli hapa???
No comments:
Post a Comment