Mpigapicha Mkongwe wa gazeti la Jambo Leo, Richard Mwaikenda, amepatwa na majonzi baada ya kuondokewa na baba yake mzazi jioni hii ya leo huko nyumbani kwake Kivule jijini Dar es Salaam. Mzee wa mpigapicha huyo alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kuwa na moyo mpana ambapo alikuwa akihudhulia Klinik katika Hospitali ya Amana, ambapo mara ya mwisho ilikuwa ni jana tu wakati alipokuwa amepelekwa hospitalini hapo na mwanae Richard, lakini kwa Bahati mbaya jioni ya leo alizidiwa na hadi ulipomkuta umauti. Akizungumza na Sufianimafoto kwa njia ya Simu jioni hii, Richard amesema kuwa msibu huo utakuwa nyumbani kwake huko Kivule na anatarajia kusafirisha msiba huo kuelekea Mkoani Mbeya kwa Mazishi hapo Keshokutwa iwapo mipango yote itakuwa imekamilika. Mwili wa Marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Amana.
BENKI YA EQUITY YAJIDHATITI KURAHISISHA USAMBAZAJI SALAMA WA MBOGAMBOGA NA
MATUNDA
-
NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
Benki ya Equity Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Rikolto pamoja na
Motley wamekuja na Bajaji ambazo zina chumba ma...
1 hour ago
No comments:
Post a Comment