Wakazi wa jijini Dar es Salaam, wakifurika kuchagua 'Key Holder' zenye majina na maana ya jina lililoandikwa katika holder hiyo iliyotengenezwa kwa kutumia kipande cha mti. Na hii ni kazi ya vijana wenye uwezo wa kufikiri na kubuni kitu kinachoweza kuonekana na kuthaminika kwa kila atakayeona kazi hiyo. Sasa watu kama hawa wanahitaji msaada mkubwa kutoka kwa Serikali ili kuendelezwa na kuweza kufanya kazi hizo kisheria na kimataifa zaidi.
Kijana Athuman Mohamed, mkazi wa Msasani jijini Dar es Salaam, aliyehitimu elimu ya msingi miaka mitatu iliyopita, akipita katika mitaa ya Posta na biashara yake ya mkono aliyoibuni kwa akili yake, akipita kutafuta wateja, mkono wa (kushoto) ni ramani ya nyumba ya ghorofa na mkono wa kulia ni basi na vyote vikiwa vimetengenezwa kwa kutumia maboksi, ambapo kila moja huuzwa kwa Sh. 5000. Kijana kama huyu anahitaji kuendelezwa kupitia Sanaa yake hii.

No comments:
Post a Comment