Gari lenye namba za usajiri T596 BPD, likiwa limepata ajali eneo la Kinondo A kwa Manyanya na dakika chache tu baada ya ajali hiyo lilikuwa ni kama linavyoonekana, hapa ni baada ya mateja ya mtaa huo kuvamia na kujisevi kila walichohitaji kabla ya kudhibitiwa na kumalizia hasira zao katika Bango la matangazo lililogongwa na gari hilo kulingoa na kutokomea nalo kusikojulikana leo asubuhi. Gari hiii iliyokuwa ikiendeshwa na mwanadada iliacha njia ghafla na kupanda ukuta huu pembezoni mwa barabara hiyo na kugonga Bango la Matangazo ya Pikpiki hadi kulivunja. Kwa bahati mdaa huyo hakupatwa na jeraha lolote zaidi ya kuchanganyikiwa na kupata akili ya haraka kushuka garini humo na kukimbilia katika duka jirani lakini vinginevyo asingeondoka eneo hilo na chochote kwa jinsi mateja ya eneo hilo yalivyo na njaa mbaya.
Gari hilo kama linavyoonekana baada ya ajali likiwa limepanda ukuta, huku baadhi ya wasamaliawema wakililinda gari hilo lisiendelee kudhuliwa na mateja.
Dereva wa gari hilo 'Mdada' akiwa katika duka alilokimbilia kujisalimisha huku akifanya mawasiliano na ndugu na jamaa.
Mateja hayo baada ya kuzuiliwa kuendelea kung'oa taa na vitu kadhaa katika gari hilo baada ya kufanikiwa kuwahi taa moja na Shoo ya mbele, hasira zao waliamua kumalizia katika bango hilo lililogongwa na gari hilo, hapa wakishirikiana kuling'oa.
No comments:
Post a Comment