Mshambuliaji wa timu ya Yanga ya Dar es Salaam, David Mwape (kushoto) na Beki wa AFC ya Arusha Amiri Msumi, wakichuana kuwania mpira, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru leo. Katika mchezo huo Yanga ilishinda mabao 6-1.
Beki wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, akipiga Krosi mbele ya Beki wa AFC ya Arusha, Salim Ngasa, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru leo.
Beki wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, akipiga Krosi mbele ya Beki wa AFC ya Arusha, Salim Ngasa, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru leo.
Kipa wa AFC ya Arusha, Said Omary, akiruka kujaribu kuokoa mpira wa Penati uliopigwa na Shadrack Nsajigwa. Penati hiyo ilitolewa baada ya beki wa AFC kumchezea rafu mshambuliaji wa Yanga, David Mwape, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment