Habari za Punde

*YANGA YALAZIMISHWA SARE YA 4-4 NYUMBANI NA DEDEBIT YA ETHIOPIA

Mshambuliaji wa Yanga, David Mwape (katikati) akiwatoka mabeki wa Dedebits Sc, Menpistu Assefa (kulia) na Birhanu Bopare, wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam jana. Timu hizo zilitoka sare ya 4-4. . Mabao ya Yanga, yalifungwa na Nadir Haroub 'Cannavaro' na Nurdin Bakar, kipindi cha kwanza, Jerry Tegete na Godfrey Bony kipindi cha pili, wakati huo huo nayo Simba ya Dar es Salaam, imetoka sare na timu ya Elan Club de Mitsoudje ya Comoro na KMKM ya Zanzibar, imechapwamabao 40 na Dc Motema Pembe ya DRC, mchezo uliochwa kwenye Uwanja wa Aman Zanzibar.
Beki wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, akicheza takoring kuokoa mpira mbele ya adui.
Goli la kwanza la Yanga lililofungwa na Nadir Haroub 'Cannavaro', mpira ukitinga wavuni na kumuacha kipa wa Dedebit, akiwa chini hoi.
Mashabiki wa Yanga, wakishangilia bao hilo ambalo hata halikuweza kudumu kwa dakika nyingi kabla ya kusawazishwa.
Kocha wa Yanga, Fredy Minziri, akiwapa Morari wachezaji wake wakati mchezo ukiendelea.
Mfungaji wa bao la 4 na la kusawazisha la Yanga, Dakika moja kabla ya mpira kumalizika, Godfrey Bony, akihojiwa na mtangazi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sport Fm Radio, Abdallah Majula, baada ya kumalizika kwa mchezo huo.
Mashabiki wakitoka uwanjani kwa unyonge baada ya timu yao kutoka sare ya 4-4.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.