Habari za Punde

*AURORA SECURITY YAWADHAMINI TAMIM NA ASHRAF, KUZICHAPA MACHI 5

Mratibu wa pambano la ngumi la Tamim na Ashraf, Shomari Kimbau, akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO, kuhusu pambano la Raundi 10 la Heavy weight, linalotarajia kufanyika machi 5 mwaka huu. Mapambano mengine yanayotarajia kuchezwa siku hiyo ni pamoja na Suleiman Said, atakayezichapa na Maneno Osward, katika uzito wa Middle, raundi 10, Benson Mwakyembe V/s Mbarouk Kheri, raundi 10, Amour Mzungu V/s Ramadhan Kiddo, raundi 10 uzito wa Tanzania Gruiserweight, na Alfonce Mchumiatumbo V/s Chukudusso, raundi 6, Heavyweight.
Mratibu wa pambano kati ya Awadhi Tamim, anayeishi nchini Sweden na Ashraf Suleiman, Shomari Kimbau, (wapili kulia) akiwatambulisha baadhi ya mabondia watakaocheza siku ya pambano hilo litakalofanyika Machi 5 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Kutoka (kushoto) ni Alfonce Mchumiatumbo, Ramadhan Kido, Seleman Said. Utambulisho huo ulifanyika kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam, leo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.