Habari za Punde

*DK. MARY NAGU USO KWA USO NA DK SLAA HOSPITALI YA AMANA

"Shida Hii ni yetu sote, kwa hili tushirikiane" Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu, akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt Slaa, wakati walipokutana nje ya Hospitali ya Amana leo mcha wakati walipofika kuwatembelea wagonjwa waliolazwa katika hospitali hiyo kutokana na kujeruhiwa na mabomu yaliyolipuka wiki iliyopita katika Kambi ya Jeshi ya 511 KJ iliyopo Gongolamboto Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu,akimjulia hali Saida Rajab, mgonjwa aliyekatika mkono wa kushoto aliyelazwa Wodi ya Mwaisela katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, baada ya kupigwa na bomu wakati wa mshike mshike uliotokea wiki iliyopita, Gongolamboto.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Willbod Slaa, akiwa na baadhi ya Wabunge wa chama hicho, katika Hospitali ya Amana kwenye moja ya wodi ya wagonjwa walioathirika na mabomu wakati walipofika kuwatembelea waathirika hao wa mabomu leo mchana.
Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu, akimjunia hali George Daud, aliyelazwa katika wodi ya Sewahaji Muhimbili kutokana na kujeruhiwa na bomu.
Ilikuwa ni ziara ya siku nzima kwa ajili ya kuwajulia hali waathirika wa mabomu, katika Hospitali za Muhimbili, Amana na Temeke, huyu pia ni mmoja kati ya waathirika hao.
Vijana wa Red Cross pia bado wapo kikazi zaidi, hapa wakipakia magodoro katika gari kutoka katika Kambi yao waliyoweka maeneo ya Mombasa kwa ajili ya kuwasaidia watoto waliokuwa bado hawajaonana na wazazi wao, ambapo hadi hii leo ni mtoto mmoja tu ndiye bado amebakia katika Kituo hicho.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.