Habari za Punde

*FAMILIA ZILIZOATHIRIKA NA MABOMU ZAZIDI KUTAABIKA GONGOLAMBOTO

Hawa ni baadi tu ya Kinamama wa familia zilizoathirika na milipuko ya mabomu ya wiki iliyopita, wakiwa nje ya mahema yao walioyojengewa kwa msaada, wakijiandalia chakula cha mchana leo, kama walivyonaswa na kamera ya Sufianimafoto. Famili kibao kwa sasa zinaendelea kuishi katika mazingira magumu ikiwa ni pamoja na kulala nje, kukosa vyoo, mahala pa kupikia na mahitaji mengine kibao kutokana na nyumba zao kubomolewa na mabomu. Serikali iwaangalie waathirika hawa kwa jicho la tatu na kwa haraka iwezekanavyo kwani leo kwao na kesho inaweza kuwa kwa mwingine.
Baadhi ya kiniamama wakiandaa mazingira ya ndani ya Hema baada ya kujengewa tayari kwa kuishi hadi hapo mambo yatakapokaa sawa.


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.