Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mzambarauni Gongolamboto, jijini Dar es Salaam, wakiwa nje ya madarasa yao baada ya kuwasili shuleni hapo leo kwa mara ya kwanza tangu ilipotokea milipuko ya mabomu katika Kambi ya 511 KJ ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) wiki iliyopita. Mahudhurio ya wanafunzi hao yamepungua tofauti na awali kutokana na hofu ya milipuko hiyo. Imeelezwa kuwa hapo awali Darasa moja lilikuwa na watoto 80, lakini leo kila darasa watoto walioripoti hawafikii hata 40, na hii inawezekana ni kwasababu ya hofu ya wazazi ambapo wengine wameamua kuwasafirisha watoto wao mikoani amba kuwahamisha shule na pengine kati ya watoto ambao hawajapatikana hadi hii leo ni miongoni mwao.
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo November 24, 2024
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam November 24,
2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na
za nyuma za M...
2 hours ago
No comments:
Post a Comment