Habari za Punde

*JAMAA AMETHAMINI NYANYA KULIKO UHAI WAKE

Mfanyabiashara wa nyanya akizoa nyanya zake zilizomwagika katikati ya Barabara eneo ya Amana Dar es Salaam leo mchana. Pamoja na kuona Roli likija mbele yake kwa kasi huku likifunga breki na kuliza Mbwa, lakini bado kijana huyo hakuthubutu kusogea pembeni kulipisha aliendelea tu na zoezi lake la kuzoa nyanya zake hadi rili lilipoamua kusimama na kumkepa huku watu waliokuwapo eneo hilo pembeni mwa Barabara hiyo, wakimpigia kelele kumuashiria aziache nyanya hizo ili kuokoa maisha yake.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.