Na Joseph Ishengoma-Maelezo
Timu ya Wataalam walioteuliwa na nchi za Uganda na Tanzania kuangalia vikwazovya usafirishaji wa mizigo ya Uganda , imependeza ujenzi wa reli kutoka bandari ya Tanga kupitia Arusha hadi Musoma kuwa itarahisisha usafirishaji wa bidhaa tofauti na hali ilivyo sasa.
Pamoja na ujenzi wa reli hiyo, timu hiyo pia imependekeza kuboreshwa bandari ya Mwambani mjini Tanga kama sehemu ya uboreshaji wa usafirishaji wa mizigo inayoelekea Uganda .
Waziri wa Uchukuzi Mhe Omari Nundu amesema hayo leo jijini Dar Es Salaam wakati akifungua mkutano wa siku moja uliojumuisha wadau wa usafirishaji wa mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam kwa kutumia reli ya Kati na barabara hadi Uganda .
Mkutano huo umejumuisha wajumbe wa Jumuiya ya Wafanyabiashara kutoka Uganda wanaopitisha bidhaa zao katika Bandari ya Dar es Salaam.
Ameseme, “mradi huu utakapokamilika utatumia dola za Kimarekani bilioni 2.7.”
Kati ya fedha hizo, dola bilioni 1.9 ni kwa ajili ya uboreshaji wa reli, dola milioni 695.5 zitaendeleza zitaendeleza bandari ya Mwambani Tanga, wakati dola milioni 72.6 zitahitajika kujenga bandari ya Musoma.
“Majadiliano kati ya serikali yatu na serikali ya Uganda kuhusu ujenzi wa mradi huu yanaendelea. Pamoja na hayo, serikali ya Tanzania inaangalia njia za kuboresha kila njia ya usafirishaji wa mizigo iki kutoa huduma bore kwa wateja wake,” amesema.
Jumuiya hiyo ya wafanyabiashara kutoka Uganda imetembelea maeneo mbalimbali ya Bandari ya Dar Es Salaam yanayohusiana na usafirishaji wa mizigo yakiwemo, kituo cha mizigo bandarini, kituo cha makonteina na kituo cha mafuta.Baadhi ya wadau wakuwa katika mkutano huo.
No comments:
Post a Comment