Habari za Punde

*20% PACENT AFUNIKA TUZO ZA KILI MUSIC AWARDS, AZOA TANO

Msanii wa maigizo, Mzee Small (katikati) akimkabidhi Tuzo Man Water, kwa niaba ya 20 Pacent, aliyeibuka kidedea katika Kategoli ya Wimbo bora wa Afro Pop, (kulia) ni Bi Chau. Msanii huyo jana katika onyesho la kutoa tuzo hizo za 'Tanzania Kili Music Awards' alifunika na kuweza kujizolea jumla ya tuzo tano na kuufanya ukumbi kuzizima kwa makelele ya kushangilia kila alipotajwa jina kushiriki katika Kategoli fulani. Hata hivyo msanii huyo hakuweza kuhudhulia onyesho hilo kutokana na kupata safari ya ghafla kulingana na maelezo ya mwakilishi wake, ambaye pia ni Producer wake Man Water. Mashabiki waliohudhulia onyesho hilo, wakishangilia baada ya kutajwa jina la 20 Pacent.
Jay Moe (wapili kushoto) JBC na Producer, wakipozi na tuzo zao baada ya kutwaa tuzo hizo jana usiku.
Khalid Chokoraa (kulia) akipokea tuzo yake ya kuwa rapa bora wa mwaka.
Mchezaji wa timu ya Yanga, Jerry Tegete (kulia) akimkabidhi tuzo ya Wimbo bora wa Raggae Dance hall, msanii C-Pwaa. Kushoto ni mchezaji wa Simba, Mussa Hassan 'Mgosi'.
Mashabiki wakipata raha ukumbini humo.
Raha zinaendelea ukumbini, mashabiki wakifuatilia kwa makini kila linalofanyika jukwaani.
Mwenyekiti wa Kamati ya ushindi ya timu ya Taifa, Rahma, naye alikuwepo ukumbini humo akipata raha kamili.
Mtangazaji wa Star Tv, Sauda Mwilima (kulia) akiwa na mwenzake wakifuatilia kwa makini.
Msanii AY, akitoa raha kamili jukwaani.
Waziri wa habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi (kushoto) akiwa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF, Angetile Osiah.
Msanii wa maigizo, Monalisa, akiwa na Alirehmtula jukwaani, baada ya kukabidhi tuzo.
Rose Ndauka, akimkabidhi tuzo ya pili C-Pwaa, baada ya kuibuka katika Kategoli ya Video bora mwaka.
Mtangazaji wa redio Times, akimkabidhi tuzo msanii Barnaba, baada ya kuibuka kidedea katika kategoli ya Wimbo bora wa Zouk Rhumba. katikati ni Mzee wa Planet Bongo, Dullah.
Msanii Linah, akiimba kwa hisia jukwaani.
Patricia Hirary, akimkabidhi tuzo, Mpoki baada ya kuibuka kidedea katika Kategoli ya Wimbo bora wa Asili na wimbo wake wa Shangazi.
Kipa wa Simba, Juma Kaseja (kushoto) akimkabidhi Tuzo Mzee Yusuph, baada ya kuibuka kidedea katika Kategoli ya Wimbo bora wa Taarab. Kulia ni beki wa Yanga, Shadrack Nsajigwa.
Mpoki akizungumza na kuwashukuru mashabiki wake baada ya kupokea tuzo hiyo.
Mapaparazi wa vyombo mbalimbali vya habari, wakiwa bize kupata picha za matukio jukwaani.
Msanii Diamond, akiimba jukwaani ikiwa ni sehemu ya burudani zilizoandaliwa usiku huo.
Waendesha shughuli Ma Mc, Millad Ayo na mwenzake wakiwajibika jukwaani.
Bi Kidude, akiwa ni miongoni mwa wasanii walioalikwa katika onyesho hilo.
Mgosi (katikati) na Tegete, wakipata menu ukumbini humo.
Wasanii wa kundi la Tanzania House of Talent THT, wakishambulia jukwaa.
Alikiba akishambulia jukwa kwa burudani kabambe.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.