Bondia Awadh Tamim, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo katika Ofisi za Kampuni ya Aurora Security, kuhusu pambano lake la ubingwa wa Afrika Mashariki na mpinzani wake Ashraf Suleiman,
lililomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita. Katikati ni Kocha wake, Juma Suleiman na Kocha msaidizi, Moses Mambo.
Tamim alielezea kuhusu pambano la ubingwa wa Afrika analotarajia kucheza mwezi Mei mwaka huu na bondia atakayepatikana katika nchi yeyote katika Afrika. Aidha Tamim aliwaondoa shaka mashabiki wake kwa kile kilichotokea ukumbini baada ya kushinda pale alipoonekana kama mtu aliyepagawa na wengi wakahisi amechanganyikiwa kutokana na mauza uza baada ya kushinda huku akipiga makelele na kuongea muda wote.
Ambapo alisema kuwa hiyo ilikuwa ni furaha kwa upande wake baada ya kumshinda mpinnzani wake kwa mara ya pili.
Baadhi ya mashabiki wa ngumi waliokuwamo ukumbini humo wakati wa pambano hilo, waliielezea Sufianifoto kile walichokiona ukumbini humo walichokiita mauzauza kuwa Tamim alifanikiwa kuubadilisha mchezo huo katika raundi ya nne baada ya Mabaunsa kumshtukia jamaa mmoja aliyekuwa chni ya jukwaa la ulingo wakati mchezo ukiendelea ambaye alichomolewa na mabaunsa na kutolewa nje juu juu.

Imeelezwa kuwa jama huyo baada ya kutolewa nje muda wote alikuwa akilia kwa sauti bila kujua sababu zilizomfanya kuwa chini ya ulingo na baada ya kutolewa nje ni sababu ipi ilimfanya alie kwa uchungu kiasi hicho.
Haya ni baadhi tu ya yaliyojili katika pambano la wababe Tamim na Ashraf, ambalo kwa kipindi kirefu Tanzania halikuwahi kutokea, Big Up nyingi kwa mdhamini wa pambano hilo aliyewezesha kumrejesha nchini Tamim ili kucheza na kumaliza ubishi.
Hapa simsemei mwingine bali ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Ulinzi ya Aurora Security, Ally Aurora, na pia wajitokeze wadau wengine wenye moyo wa kuendeleza mchezo huu nchini ili nasi tuweze kufikia hatua za kimataifa zaidi.
No comments:
Post a Comment