Na Mwandishi Wetu
KAMATI ya Utendaji ya Shirikishola Ngumi za Ridhaa Tanzania
(BFT), jana imekutana na mabondia wa timu ya Taifa katika ofisi za Shirikisho hilo pamoja na kocha msaidizi Benjamin Mwangata.
Lengo la kikao hicho ni mabondia kukutana na wajumbe wa kamati hiyo ili kufahamiana na kufahamu jukumu lao kama mabalozi ambao
wataiwakilisha nchi katika mashindano mbalimbali ya
kimataifa.
Akizungumza na mabondia hao, Katibu Mkuu wa BFT, Makore
Mashaga alisema, mafanikio ya mchezo huo yanahitaji nidhamu ya bondia, uzalendo na kujituma katika mazoezi na mashindano.
Alisema hivi sasa, BFT inatarajia kupeleka mabondia katika
mashindano ya Majiji ambayo yatafanyika Kampala nchini Uganda kuanzia Aprili mosi
hadi tatu mwaka huu.
Aliongeza kuwa, mashindano hayo ni kipimo kizuri kwa mabondia hao kabla ya ushiriki wao katika mashindano makubwa ya afrika
ambayo yamepangwa kufanyika Maputo, Msumbiji Septemba mwaka huu.
Alisema umefika wakati wa mabondia, kutanguliza uzalendo
katika na kudumisha nidhamu ili kufikia lengo la walilonalo kama
mabalozi wa Tanzania katika mashindano mbalimbali,
Kwa upande wao, mabondia hao waliipongeza BFT kwa kuachagua
mabondia wenye uwezo na sifa ya kuiwakilisha nchi katika mashindano mbalimbali ya kimataifa.
Walisema mpango wa BFT kuuingiza mchezo huo katika mpango wa polisi amii, utawezesha kupatikana kwa wahusika wa biashara hiyo
pamoja na watumiaji ili wafikishwe katika vyombo vya sheria.
“Sisi kama mabalozi wa Tanzania katika mchezo huu, tuna
uhakika mkubwa wa kurudi na medali katika mashindano ya kimataifa pamoja na haya ya
majiji,” alisema Seleman Kidunda kwa niaba ya mabondia hao.
Alisema pamoja na changamoto zinazolikabili shirikisho hilo, wapo
tayari kufanya mazoezi katika mazingira magumu ili waweze
kupeperusha bendera ya nchi katika mashindano ya majiji.
Mabondia hao, wanatarajia kuanza mazoezi leo katika uwanja
wa ndani wa Taifa lakini bado wanakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa vifaa na mahitaji mengine kama maji, chakula na nauli.
BFT inatoa wito kwa taasisi, kampuni na wadau wengine wa
michezo kuiwezesha timu hiyo ili iweze kufanya mazoezi yake katika mazingira mazuri.

No comments:
Post a Comment