Waziri wa Habari,, Vijana Utamaduni na Michezo, Dkt. Emmanuel Nchimbi, (wapili kushoto) akiwa meza Kuu na Mwenyekiti wa Chama cha Waandsihi wa Habari (TASWA), Juma Pinto (wakwanza kushoto) na aliyekuwa mpigapicha wa Habari Leo Athuman Hamis, wakati alipofika katika Ufukwe wa Cine Club kuwa mgeni rasmi kwenye Bonanza la TASWA lililokuwa maalum kwa ajili ya waandishi wa habari lililofanyika jana. Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari, wakichuana katika kukimbia mbio za mita 100, ambapo mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, Absolomon Kibanda, aliibuka kidedea baada ya kuwamwaga wahariri wenzake.
Wengine, walikuwa ufukweni wakipata upepo wa Bahari tu kutokana na kutokuwa na mazoea ya kushiriki katika michezo yeyote.
Baadaye ilikuwa ni mbio za waandishi wa kike na katika mbio hizo, Samirah Kiango wa Uhuru Redio aliibuka kidedea.
Wengine, walikuwa ufukweni wakipata upepo wa Bahari tu kutokana na kutokuwa na mazoea ya kushiriki katika michezo yeyote.
Baadaye ilikuwa ni mbio za waandishi wa kike na katika mbio hizo, Samirah Kiango wa Uhuru Redio aliibuka kidedea.
Hata Mashalobalo pia walikuwepo si unamcheki jamaa huyu alivyotinga Jinzi lake huku akipata Biere kimtindo kwa staili yake na mkononi akiwa na akiba ya chupa mbili za Ndovu wakati anayokunywa ni Tusker, sasa sijui mchanganyiko huu ni kwa sababu ni bia za bure ama vipi, Mashalobalo wanamambo!
Na baadaye ilikuwa ni burudani ya Misebene kwa kwenda mbele, hapa wakiserebuka..
Hapa ni Sufianimafoto, akiyarudi masebene na mchekeshaji wa Ze Commedy wa Chanel5, Masawe Mtata A.K.A Kicheko wakati wa Bonanza hilo.
Kicheko akipozi na Manzie fulani hivi sijui kama ni Manzie wake ama ni naniliu wake...
Kila mtu alikuwa na staili yake ya kucheza masebene katika Bonanza hilo kama unavyowacheki jamaa hawa akiserebuka kana kwamba wanacheza ngoma ya Kizaramo ama Mdumange.
Kuonyesha kuwa jamaa huyu hachezi mbali na Biere, alikuwa haachi bia zake mezani kama walivyokuwa wakifanya wenzake, yeye ilikuwa ni kunywa popote awapo, hamuamini mtu katika meza yao.
Wengine walikuwa wakijiona kama kina Aisha Madinda, hapa wakisakata Alaji Alaji.
Wengine walikuwa katika meza zao tu wakikata Biere kama meza hii si unaicheki ilivyosheheni??
Mtangazaji Chanel 5, Patrick Nyembela, akipozi kwa picha na Miss Linda.
Wahariri wa magazeti ya Kampuni ya The Guardian, kutoka (kushoto) ni Mhariri wa Michezo wa Gazeti la Nipashe, Amour Hassan, Joseph Kapinga na Fredy Ogoti, wakipozi kwa picha.
Wasebeneka kati...
Japo wangine walikuwa kazini wakipiga picha lakini hawakuthubutu kuacha chupa zao za Biere chini, kama jamaa huyu yeye kaikumbatia chupa yake.
Mwimbaji wa Twanga, Charls Baba, akiwachezesha wanenguaji wa bendi hiyo kwa rap wakati wakitoa shoo mbele ya waandishi wa habari jana.
Mhhh! kama kawaida ya jamaa huyu, sijui hapa alikuwa akizisalia Biere hizi ama vipi, lakini hapa ni wakati akiwa Dansing Floo, akisakata sebene.
"POMBE SIO CHAI UKIZIKOMOA ZINAKUKOMOA"
"POMBE SIO CHAI UKIZIKOMOA ZINAKUKOMOA"
Jamaa huyu aliyetambulika kwa jina moja la 'Mpingo' wala si mwandishi wa habari bali ni Kanjanja aliyezamia tu shughuli hii ambayo wala ilikuwa haimuhusu, akitambaa baada ya kushindwa kusimama na kutembea kutokana na kulewa chakali kwa kunywa mipombe bila kujipimia.
Hapa akitambaa kuingia katika moja ya kibanda kupumzika.
Wengine nao wailamua kujificha nyuma ya mabango ili wasionekane baada ya kuzidiwa na Pombe, Jamaa huyu yeye alikuwa akitokwa na udenda na jasho huku akikoroma muda wote aliolala huku nyuma ya Bango hili.
No comments:
Post a Comment