Meneja wa Tawi la Kampuni ya Ulinzi ya Aurora Security Mkoa wa Tanga, Hemed Aurora (kuli) akimvisha mkanda wa Ubingwa wa Afrika Bondia Awadh Tamim, baada ya kushinda pambano lake na Ashraf Suleiman, lililofanyika kwenye Ukumbi wa DDC Mliman City Mwenge jijini Dar es Salaam jana, Tamim alishinda pambano hili katika raundi ya saba kwa Knockout. Wapili (kushoto) ni mratibu wa pambano hilo , Shomari Kimbau.
Mabondia Ashraf Suleiman (kushoto) na Awadh Tamim, wakipongezana ikiwa ni sehemu ya kuonyesha ‘Fair Play’ baada ya kumalizika kwa mpambano huo. Kulia ni Meneja wa Tawi wa Kampuni ya Aurora Security Mkoa wa Tanga, Hemed Aurora.
Bondia Ashraf Suleiman, akihojiwa na waandishi wa habari baada ya kumalizika mpambano huo, ambapo alisema kuwa kwa upande wake amekubaliana na matokeo hayo na kumpa Big Up mpinzani wake Tamim, kwa kumaliza pambano hilo. "Nampa Big Up sana Tamim kwani ameweza kuonyesha uwezo wake, na pia namsifu kwa kuwa na pumzi ya kutosha kuweza kunizidi mimi ambaye kwa kweli nilichoka kama yeye lakini mie naona nilikuwa zaidi,
Nawahasa waandaaji na mapromota wa Tamim, wamuendeleze ili aweze kufika mbali kwani ni bondia mzuri na mwenye roho ya paka, kwani sikujua kama angeweza kufika hata raundi ya nne kutokana na Panchi nilizokuwa nikimpa hadi kumpeleka chini mara mbili lakini bado aliamka na kuendelea, naye kufanikiwa kunipeleka chini, kwa matokeo haya mie nimeridhika nayo kabisa wala sina tena ubishi amenishinda" alisema Ashraf.
Tamim (kulia), akimpeleka chini Ashraf kwa konde zito.
Mwamuzi wa mchezo huo, akimzuia Ashraf ili kumnusulu, Tamim, baada ya kupigwa konde zito lililompeleka chini.
Mwamuzi akimwesabia Tamim, baada ya kupelekwa chini.
Bondia Awadh Tamim (kushoto) akimshambulia mpinzani wake, Ashraf Suleiman, kwa konde zito wakati wa pambano lao la Ubingwa wa Afrika lililofanyika jana kwenye Ukumbi wa DDC Mlimani City Mwenge jijini
Bondia Awadh Tamim (kulia) akimshambulia mpinzani wake, Ashraf Suleiman, kwa konde zito wakati wa pambano lao la Ubingwa wa Afrika lililofanyika jana kwenye Ukumbi wa DDC Mlimani City Mwenge jijini Dar es Salaam . Katika pambano hilo , Tamim alishinda kwa Knockout katika raundi ya saba.
Mkanda wa Ubingwa ukipelekwa Ulingoni na Mrembo.
Mashabiki wa Ashraf, wakishangilia ukumbini kwa mbwembwe kabla ya kuanza kwa pambano hilo.
Mgeni rasmi katika pambano hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charls Kenyela Watatu (kushoto) Msemaji wa TFF, Boniface Wambura (kushoto) Meneja wa Tawi la kampuni ya Aurora, mkoa wa Tanga, Hemed Aurora (wapili kushoto) Mratibu wa pambano hilo, Shomari Kimbau (katikati) Bondia Rashid Matumla na Mwongozaji wa shughuli hiyo, Mc, wakiwa kimya wakati wakiomba dua maalum kwa ajili ya watu wa Gongolamboto, kabla ya kuanza pambano hilo.
ZOLA D AKIMBIWA NA MPINZANI WAKE KIZA KINENE
Bondia wa mchezo wa Mix Fight, Zola D, akishuka ulingoni bila kupigana baada ya mpinzani wake Kiza Kinene kuingia mitini na kumfanya kupewa ushindi wa chee.
Mashabiki wa Zola D, wakimshangilia wakati akishuka ulingoni kwa kukimbiwa na mpinzani wake.
Sufianimafoto (kulia) akipozi kwa picha na Masanja Mkandamizaji, wakati wakifuatilia mapambano hayo ukumbini.
MAPAMBANO YA UTANGULIZI
Mabondia Ramadhan Kido (kushoto) na Alfonce Mchumiatumbo, wakipambana katika pambano lao la utangulizi lisilo la ubingwa na raundi 6, wakati wa pambano la Ubingwa wa Afrika kati ya Awadh Tamim na Ashraf Suleiman, lililofanyika kwenye Ukumbi wa DDC Mlimani City Mwenge jijini Dar es Salaam jana. Katika pambano hilo Mchumiatumbo, alishinda kwa pointi.
Mabondia Shadrack Ignase (kushoto) na Allan Kamote kutoka Tanga, wakipambana katika pambano lao la utangulizi lisilo la ubingwa na raundi 6, wakati wa pambano la Ubingwa wa Afrika kati ya Awadh Tamim na Ashraf Suleiman, lililofanyika kwenye Ukumbi wa DDC Mlimani City Mwenge jijini Dar es Salaam jana. Katika pambano hilo Kamote, alishinda kwa pointi.
No comments:
Post a Comment