Tsunami Japan baada ya tetemeko kubwa
Tetemeko kubwa la ardhi limepiga kaskazini-mashariki mwa Japan, na kuibua mawimbi ya tsunami ambayo yamesababisha hasara kubwa.
Hadi sasa wakazi wa mji huo wamebaki katika maofisi yao kutokana na nyumba zao kusombwa na maji na nyingine kuendelea kutikisika huku nyingi zikisombwa na maji.
Kwa tukio hilo, tayari nchini Kenya wananchi wamepewa tahadhali ya kutokuwa maeneo ya Ufukwe wa Bahari ya Hindi kwani inaweza kutokea yale yaliyokwisha tokea miaka ya nyuma.
Televisheni nchini Japan, imeonesha magari, meli na hata majengo makubwa yakizolewa na mawimbi makubwa ya maji ya bahari baada ya tetemeko lenye ukubwa wa 8.9 kupiga.
Tetemeko hilo pia limesababisha moto katika maeneo mengi ya Japan ukiwamo mji mkuu Tokyo, ambapo imearifiwa watu 15 wamekufa.
Tetemeko hilo limepiga kiasi cha kilometa 400 kutoka mji mkuu na mawimbi yadaiwa kuingia umbali wa maili 20 ndani ya mji.
Wataalam wa matetemeko wamesema hili ni moja ya tetemeko kubwa kuipiga Japan kwa miaka mingi.
Wakati tetemeko lilipopiga, majengo mjini Tokyo yaliyumba. Mtu kutembea ilikuwa sawa na kuwemo ndani ya meli inayopigwa mawimbi baharini.
Watu walishuka chini kutoka katika ofisi zao na kusalia mitaani wakiwa wanatetemeka.
Moto mkubwa ulizuka katika eneo moja la mji na katika maeneo mengine, watu waliojeruhiwa walitolewa nje ya vituo.
Mara moja serikali ilitoa onyo la tsunami.
Katika mji mkuu Tokyo, usafiri wa umma umesimamishwa, lifti katika majengo mengi zimezimwa na maelfu ya watu wamekusanyika katika bustani za wazi na vituo vya treni.
Onyo la tsunami limetolewa pia katika maeneo yote ya bahari ya Pacific ikiwemo Philippines, Indonesia, Taiwan, Hawaii, na mwambao wa bahari ya Pacific nchini Urusi na kaskazini mwa Amerika Kusini.
Mawimbi makubwa yalipiga katika miji ya Miyagi na Fukushima, na kuharibu vibaya sehemu kubwa ya makazi ya watu eneo la pwani. Shirika la habari la Kyodo limesema mawimbi yaliyofikia urefu wa mita 10 na kupiga bandari ya Sendai huko Miyagi .
TAHADHALI:- Kutokana na tukio hilo, basi hata wananchi wa Tanzania tusidhalau pia tuchukue tahadhali kwa kutokuwa maeneo ya Ufukwe wa Bahari ya Hindi.
Na hasa ukizingatia leo ni ile siku maalum ya waandishi wa habari kukutana katika ufukwe wa Bahari ya Hindi eneo la CINE CLUB, katika Bonanza la Taswa, inabidi kuchukuliwa tahadhali za haraka kuhusiana na hili.
Na pia katika ufukwe wa Coco Beach pia kutakuwa na Tamasha la Tigo katika shughuli za Promosheni ambapo watu kibao hukusanyika kwa ajili ya kupata burudani kutoka kwa wasanii wa Muziki wa Bongo Fleva, nao wachukue tahadhali.
No comments:
Post a Comment