"Watanzania kupata msaada wa kisheria kupitia simu zao za mikononi"
Na Mwandishi wa Sufianimafoto
MTANDAO wa Mashirika yanayotoa Msaada wa kisheria Tanzania (TANLAP) kwa kushirikiana na Kampuni ya Push Mobile, wamezindua huduma ya Sheria Kiganjani ambayo inatoa fursa kwa watanzania kupata huduma za kisheria kwa kupitia ujumbe mfupi wa simu ya mkononi.
Mkurugenzi Mtendaji, TANLAP , Deonatus Mutani, alisema kuwa huduma hiyo ina lengo la kusogeza haki karibu na jamii na kuongeza kuwa huo ni mwanzo wa zama ambapo matumizi ya teknolojia ya habari yanaelekea kuwezesha upatikanaji wa taarifa na elimu ya misingi ya kisheria kupitia simu ya mkononi.
Mutani alisema kuwa mtu yeyote anayetaka kupata huduma ya Sheria Kiganjani anatakiwa kutuma
neno "sheria" kwenda namba ya simu 15551 na baadaye atapata idadi aitakayo ya ujumbe mfupi wenye kuelimisha juu ya masuala mbalimbali ya kisheria.
neno "sheria" kwenda namba ya simu 15551 na baadaye atapata idadi aitakayo ya ujumbe mfupi wenye kuelimisha juu ya masuala mbalimbali ya kisheria.
Alisema kuwa lengo jingine la huduma hiyo ni kuongeza ufahamu wa wananchi juu ya huduma ya msaada ya wa kisheria, kuendeleza elimu ya kisheria na kuhamasisha upatikanaji rasilimali za kuimarisha na kuboresha huduma za msaada wa kisheria na elimu ya kisheria katika Tanzania.
“Uelewa mdogo wa kisheria kwa walengwa na wadau wa msaada wa kisheria ni moja ya changamoto
zilizopelekea kuundwa TANLAP ili kuweza kukabiliana na changamoto hii, TANLAP imeungana mkono na taasisi ya Push kubuni, kuanzisha na kuendeleza huduma ya Sheria Kiganjani,” alisema Mutani.
zilizopelekea kuundwa TANLAP ili kuweza kukabiliana na changamoto hii, TANLAP imeungana mkono na taasisi ya Push kubuni, kuanzisha na kuendeleza huduma ya Sheria Kiganjani,” alisema Mutani.
Alisema kuwa anaamini upatikanaji wa haki kwa watu maskini na jamii zinazoishi katika mazingira hatarishi kama vile watu wenye ulemavu, watu wanaoishi katika maeneo yasiyofikika kwa urahisi, na hasa maeneo ambako sio rahisi kupata huduma za ushauri wa kisheria.
Aliongeza kuwa wananchi wa Tanzania wana haki ya kuwa na ufahamu wa sheria na katiba, ufahamu wa haki na majukumu yao, ili kuwawezesha kupata huduma za kisheria zilizo bora na
kwa wakati.
kwa wakati.
Alisema kuwa TANLAP imeandaa jumbe fupifupi zaidi ya 2,000 zinazohusu mada mbalimbali za kisheria kama vile ardhi, migogoro ya ndoa, mirathi, ulinzi wa watoto, haki za binadamu,
haki za walaji, migogoro ya makazi, masuala ya mazingira, haki za makabila madogo na migogoro ya kazi.
haki za walaji, migogoro ya makazi, masuala ya mazingira, haki za makabila madogo na migogoro ya kazi.
Pia wameandaa huduma za kisheria za usalama barabarani, haki na wajibu wa wakimbizi, katiba,
na mambo mengine ya kisheria ambayo yanagusa maisha ya kila siku ya Watanzania.
na mambo mengine ya kisheria ambayo yanagusa maisha ya kila siku ya Watanzania.
Kampuni ya Push itawasilisha jumbe hizi kwa watu wengi kadiri iwezekanavyo.
No comments:
Post a Comment