Habari za Punde

*KITUO CHA SUPER SPORT CHAZIPA BIG UP YANGA NA SIMBA

KITUO cha televisheni cha Super Sport kimezipa nafasi ya kwanza katika Bara la Afrika kwa upinzani wa jadi timu za Yanga na Simba.

Msimamizi wa kituo hicho, Trevor Tachiona, alisema hayo wakati wakitoa mafunzo maarumu kwa wafanyakazi wa kituo cha Star TV siku ya Jumamosi na timu hizo kutoka sare ya bao 1-1.

Tachiona, alisema kuwa wameziweka timu hizo katika nafasi ya kwanza kutokana na idadi ya watu wanaofika uwanjani kulinganisha na timu nyingine zenye upinzani wa jadi barani Afrika.

Alisema kuwa katika uzoefu wake, Yanga na Simba zimevuta mashabiki wengi, kuzidi mechi za timu nyingi kongwe barani Afrika. Alisema kuwa hata timu za Orlando Pires na Kaizer Chiefs za Afrika Kusini, Al Ahly na Zamalek hazifikii upinzani wa Simba na Yanga.

Alifafanua kuwa ikiwa ni mara yake ya pili kuhudhuria mechi ya Yanga na Simba, hajawahi kuona msisimko mkubwa wa mashabiki tokea asubuhi, wakati wa mechi na hata baada ya mechi.

Alisema kuwa hata upande wa mavazi nao umemvutia sana kwani mashabiki wengi walivaa jezi zinazofanana na rangi ya timu zao,

Pia alisema upande wa ukaaji nao ulikuwa wa mipaka, hakuna mpenzi wa timu anayekaa kwenye jukwaa la timu pinzani kama ilivyo Afrika Kusini.
KITUO cha televisheni cha Super Sport kimezipa nafasi ya kwanza katika bara la Afrika kwa upinzani wa jadi timu za Yanga na Simba.

Msimamizi wa kituo hicho, Trevor Tachiona alisema hayo wakati wakitoa mafunzo maarufu kwa wafanyakazi wa kituo cha Star TV siku ya Jumamosi na timu hizo kutoka sare ya bao 1-1.

Tachiona alisema kuwa wameziweka timu hizo katika nafasi ya kwanza kutokana na idadi ya watu wanaofika uwanjani kulinganisha na timu nyingine zenye upinzani wa jadi barani Afrika.

Alisema kuwa katika uzoefu wake, Yanga na Simba zimevuta mashabiki wengi, kuzidi mechi za timu nyingi kongwe barani Afrika. Alisema kuwa hata timu za Orlando Pires na Kaizer Chiefs za Afrika Kusini, Al Ahly na Zamalek hazifikii upinzani wa Simba na Yanga.

Alifafanua kuwa ikiwa ni mara yake ya pili kuhudhuria mechi ya Yanga na Simba, hajawahi kuona msisimko mkubwa wa mashabiki tokea asubuhi, wakati wa mechi na hata baada ya mechi.

Alisema kuwa hata upande wa mavazi nao umemvutia sana kwani mashabiki wengi walivaa jezi zinazofanana na rangi ya timu zao,

Pia alisema upande wa ukaaji nao ulikuwa wa mipaka, hakuna mpenzi wa timu anayekaa kwenye jukwaa la timu pinzani kama ilivyo Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.