Habari za Punde

*LUKUVI ATUA LOLIONDO KWA BABU, AKUKAGUA MTI WA DAWA, APATA KIKOMBE

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Williamu Lukuvi, akiwa ameshika tawi la mti aina ya Mugamuryaga ambao huchimbwa mizizi yake na kuchemshwa dawa. Pembeni ni Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Elias Wawalali, wakati alikuwa akimuonyesha mti huo.

Mchungaji Mstaafu Ambilikile Masapile akimgawia dawa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), William Lukuvi na Rosemary Nyerere, baada ya Lukuvi kumaliza kuukagua mtu unaozalisha dawa hiyo. Lukuvi alitua Loliondo mwishoni mwa wiki iliypita.

Baadhi ya wananchi waliofika nyumbani kwa Mchungaji Mstaafu Ambilikile Masapile kunywa dawa, wakiagana na Mchungaji na kumtakia kheri baada ya kupata kikombe.Kulia kwa Mchungaji ni Balozi Paul Rupia.

Sehemu ya msululu wa foleni ya magari yaliyokatiza Mto katika Kijiji cha Samunge.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.