Habari za Punde

*MBUNGE ATINGA BUNGENI AKIWA AMEVAA HERENI, ATIMULIWA UKUMBINI

MBUNGE anayedaiwa kuwa kijana kuliko wote kati ya wabunge wa Bunge tukufu la nchini Kenya, Gideon Mbuvu ametimuliwa kutoka ndani ya ukumbi wa bunge baada ya kutinga ukumbini humo akiwa ametinga mavazi ya kibitozi na heleni.

Mbunge huyo alifukuzwa kwenye kikao cha juzi akiwa amevaa miwani ya jua na hereni ndogo za madini yenye thamani kubwa na kuwafanya wabunge wenzake kubaki wakimshangaa wakati akiingia ukumbini humo.

Naibu Spika wa Bunge hilo, Farah Maalim, alisema Mbunge huyo jinsi alivyoingia ukumbini na mavazi hayo haionyeshi heshima kwa bunge, ambalo halijawahi kuwa na mbunge mwanamume aliyewahi kuvaa hereni.

Mbunge huyo Mbuvi mwenye umri wa miaka 35, anayejulikana kwa jina maarufu la kitaani ‘Sonko’ jina hilo likiwa na maana ya mtu Tajiri mwenye maisha ya kifahari, alisababisha kelele kubwa wakati alipokuwa akiingia ukumbini humo juzi.
Maalim, alisema katika historia ya bunge hilo ni mara ya kwanza kwa mheshimiwa mbunge anayevaa vitu vya ajabu ajabu, kitu ambacho kimepingwa na wafuasi wa mbunge huyo.

“Staili ya maisha ya ‘Sonko’ ni ya kuvaa vyema kwa kuupamba mwili wake hata kwa suti za kimichezo na ndiyo kitu unachokishuhudia leo”, mbunge mmoja alisema.
Mbunge huyo katika kujitetea kutokana na mavazi yake hayo, alisema kuwa yeye anawakilisha vijana na ndiyo maana ameamua kutinga mavazi hayo.

Hata hivyo utetezi huo ulipingwa na mbunge mmoja aliyesimama na kusema kuwa “Mbona mimi katika Jimbo langu niko na Vijana kibao na hawavai hizo maeleni”? alihoji mbunge huyo

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.