Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Taasisi ya Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi Serikalini (GEPF), Anselim Peter (wapili kulia), Meneja wa Masoko na Utekelezaji, Aloyce Ntukamazina (katikati) na Ofisa Uendeshaji Mwandamizi wa mfuko huo, Salma Mtaullah, wakiwakabidhi msaada wa vyombo Naibu Kamanda wa Kikosi cha 511 KJ, Meja Samwel Magile kwa niaba ya askari wasiooa na wasioolewa (Makapela) na Elizabeth Michael, aliyepokea kwa niaba ya Umoja wa Wake wa Wanajeshi wa Kikosi cha 511 KJ, (UWAKE), walioathirika na mabomu. Ujumbe wa Mfuko huo ulifika kambini hapo Gongolamboto Dar es Salaam leo na kutoka msaada huo kwa ajili ya askari makapela wanaoishi katika kambi hiyo na wake wa wanajeshi waishio katika kambi hiyo.
Naibu Kamanda wa Kikosi cha Jeshi la Wananchi cha 511 KJ cha Gongolamboto, Samwel Magile, akizungumza jambo na wafanyakazi wa Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi Serikalini (GEPF) wakati walipofika kambini hapo leo mchana kwa ajili ya kutoa msaada wa vyombo kwa wake wa wanajeshi, ambao ni wanachama wa mfuko huo pamoja na askari wasiooa na kuolewa (Makapela) wanaoishi katika kambi hiyo.

Meneja wa Masoko na Utekelezaji wa Mfuko huo, Aloyce Ntukamazina (katikati), akisaidiana na askari hao kushusha na kubeba vyombo hivyo kwa ajili ya kuanza zoezi la kuwakabidhi.
JAPAN NAO WAGUSWA NA KUTOA MSAADA KWA WAATHIRIKA LEO
Mchungaji, Joshua Lee kutoka Jumuiya ya Korea (kulia) akimkabidhi sehemu ya msaada wa vijimfuko vya unga 715 vya Kg 10 kila kimoja na nguo 150, Mkurugenzi Msaidizi wa Manispaa ya Ilala, Gabriel Fuime, kwa ajili ya wakazi wa Gongolamboto walioathirika na mabomu, msaada huo unathamani ya Sh. milioni 6. Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Korea nchini Tanzania, Haemyung Rheo.
TPB NAO WATOA MSAADA KWA WAATHIRIKA
Kaimu Katibu Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania, Kasmir Nkuba, akimabidhi msaada wa vitu mbalimbali, Mkurugenzi Msaidizi wa Manispaa ya Ilala, Gabriel Fuime, kwa ajili ya Waathirika wa Mabomu wa Gongolamboto. Makabidhiano hayo yalifanyika leo mchana kwenye Ofisi ya Katibu Kata Gongolamboto. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Benki ya Posta Tanzania, Noves Moses.
No comments:
Post a Comment