Habari za Punde

*WAFANYABIASHARA WA SOKO LA URAFIKI WAANZA UJENZI KUGANGA NJAA

Wafanyabiashara wa soko la Mahakama ya Ndizi Urafiki, waliobomolewa vibanda vyao jana, leo wameanza ujenzi wa kinyemela kwa ajili ya kuendelea na biashara kwa kile wanachaomini kuwa Serikali imefanya makosa kubomoa soko hilo hali ya kuwa ilitumia gharama kubwa ya karubu milioni 8 na ushehe kujenga soko hilo na kuzinduliwa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa kipindi hicho na kuzialika bendi za Msondo na Sikinde kuzindua soko hilo, cha kujiuliza je Serikali haikujua kuwa eneo hilo si maalum kwa matumiszi ya soko hadi ikatumia gharama hiyo?. Wafanyabiashara hao wamesema kuwa hawataondoka eneo hilo hadi watakapohakikishiwa kulipwa fidia ya mali zao zilizopotea na hasara kubwa waliyoipata na wanayoendelea kuipata kutokana na kukaa bila kazi toka jana.


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.