Msanii wa muziki wa Injili, Miriam Lukindo, akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo mchana kuhusu Tamasha la uzinduzi wa Video ya wimbo wake wa 'Ni Asubuhi', inayotarajia kuzinduliwa Aprili 10 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee. Kushoto ni Mratibu wa uzinduzi huo, John Momadi na.
Na Sufianimafoto Reporter, jijini
Msanii wa muziki wa Injili nchini maarufu kama Miriam Lukindo, leo ametangaza rasmi uzinduzi wa Video ya wimbo wake wa Ni Asubuhi, uzinduzi utakaofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam April 10 mwaka huu.
Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa Habari leo mchana katika Ukumbi wa Hadees, Miriam alisema kuwa maandalizi ya uzinduzi huo yamekamilika ikiwa ni pamoja na wasanii watakaosindikiza uzinduzi huo.
Miriam aliwataja wasanii wa muziki wa Injili wanaotarajia kusindikiza uzinduzi huo kuwa ni pamoja na Marion Shako kutoka nchini Kenya, pamoja na wasanii wengine wa muziki wa injili kutoka nyumbani kama, Upendo Nkone, Martha Mwaipaja, Jane Misso, Jackson Benti na Christina Shusho.
Aidha alisema kuwa pia kutakuwa na makundi maarufu mbalimbali ya Kwaya yatakayotoa burudani kama Kinondoni Revaivel, KKKT Sinza, Living Water, DPC Woship Team pamoja na kundi maarufu la The Voice.
Viingilio vya Tamasha hilo ni Sh. 10,000 kwa watu wa VIP na Sh. 5,000 kwa watu wa kawaida.

No comments:
Post a Comment