Habari za Punde

*NEW HABARI YATOKA SARE YA 1-1 NA WAPYA WA STAR TV

Kikosi cha timu ya Kampuni ya New Habari Fc, katika picha ya pamoja kabla ya kuanza mchezo wa kirafiki na Star Tv, mchezo ulifanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Kijitonyama juzi. Timu hizo zilitoka sare ya kufungana 1-1, huku New habari ikiwa ya kwanza kupata bao kupitia kiungo wake, Jonathana Tito, aliyeachia shuti kali lililomshinda kipa wa Star na kugonga mlingoti wa kushoto na kisha kutinga wavuni.
Star waliweza kusawazisha bao hilo dakika 1 kabla ya mapumziko kupitia mchezaji wao ambaye hawakutaka kumtaja jina kama ambavyo walikuwa wakiitana uwanjani humo, "Father" "Oya". Star walikuwa wakiongozwa na wachezaji wengi vijana ambao walionekana kuwa si wafanyakazi wa kituo hicho lakini bado New habari walionekana kuumudu mchezo huo na kuwapeleka puta huku muda wote wakifika katika lango lao.
Kikosi cha Star Tv HAPA vipi?, wangapi tunaofanyanao kazi mtaani, NSSF ya mwaka huu ipo kazi.


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.