Eneo la lilipokuwa Soko la Mahakama ya Ndizi Urafiki linavyoonekana baada kubomolewa vibanda vya soko hilo ambapo kazi ya ubomoaji wa vibanda hivyo ilianza usiku wa kuamkia leo majira ya saa tisa. Wafanyabiashara wa eneo hilo wamelalamikia utaratibu huo wa ubomoaji kwa kudai kuwa hawakutaarifiwa kuwa zoezi hilo lingefanywa muda huo na kusababisha hasara kubwa na upotevu wa mali za wafanyabiashara waliokuwa na vibanda vyao eneo hilo. Hata hivyo zoezi hilo lilichukua sura mpya leo mida ya saa nne asubuhi baada ya wafanyabiashara hao kufika na kukuta hali hiyo na kuamua kufanya vurugu kwa kuziba barabara hiyo kwa kuweka mawe na magogo Barabarani na kuzuia magari kupita eneo hilo huku baadhi yao wakivunja vioo vya magari hali iliyopelekea askari Polisi kufika eneo hilo haraka na kufanya kazi ya kuondoa vizuizi hivyo wenyewe na kuruhusu magari yaliyokuwa tayari yamefungamana kwa foleni kutokana na yote kupita katika njia moja kuanza kupita.
Askari Polisi waliovalia kiraia wakiondoa takata zilizokuwa zimewekwa barabarani na wafanyabiashara hao ili kuzuia magari kupita eneo hilo leo asubuhi.
Askari Polisi waliovalia kiraia wakiondoa takata zilizokuwa zimewekwa barabarani na wafanyabiashara hao ili kuzuia magari kupita eneo hilo leo asubuhi.
Askari hao wakiendelea na zoezi la kuondoa takataka katikati ya Barabara.
Hali haikuwa ya kawaida mahala hapa kutokana na wafanyabiashara hao kuwa na hasira zaidi kutokana na kupata hasara ya kupotelewa na mali zao ambazo imeelezwa usiku huo walionekana vijana wakifanya kazi ya kujisevia wakati zoezi hilo likiendelea, hali iliyopelekea hali hii ya kuziba Barabara kwa kutumia vitu kama hivi anavyoondoa askari huyu. Askari Polisi wakiwadhibiti baadhi ya vijana waliowakamata wakati wa sakata hilo.
Wengine walionekana wakiwa bize kujaribu kuhamisha vitu vyao kama jamaa huyu akiwa bize kusukuma Guta lililosheheni biashara yake ya mitumba kutoka mahala hapo. Wakishirikiana kuondoa magogo ya nguzo za umeme yaliyokuwa yamewekwa katikati ya Barabara hiyo ili kuzuia magari kupita.
Askari wakilinda usalama baada ya kuondoa vizuizi barabarani na kuanza kuruhusu magari kupita eneo hilo.

No comments:
Post a Comment