Kampuni ya Bia Tanzania TBL, imekamilisha pilika pilika zote za maandalizi ya onyesho la kutoa Tuzo za Muziki za Kili 2011, kupitia kinywaji chake cha bia ya Kilimanjaro Premium Lager, onyesho linalotarajia kufanyika siku ya jumamosi Machi 26 mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za TBL leo mchana, Mkurugenzi Masoko wa kampuni hiyo, David Minja, alisema kuwa maandalizi ya onyesho hilo yamekamilika na kuwataja wasanii watakaotoa burudani katika onyesho hilo.
Aliwataja wasanii hao kuwa ni pamoja na Joe Makini, Stara Thomas, Banana Zorro, Diamond, C-Pwaa, 2% Pacent, Linah, Mzee Yusuph, Mapacha 3 na kundi zima la Tanzania House Of Talent THT.
Aidha Minja, alisema kuwa, katika onyesho la utoaji wa Tuzo za mwaka huu mbali na kupambwa na burudani tofauti kutoka kwa wasanii mbalimbali, pia mwaka huu onyesho litakuwa na mvuto zaidi na madiliko ukilinganisha na maonyesho yaliyopita kutokana na kuboresha katika baadhi ya mambo.
“Tumekuwa tukidhamini Tuzo hizi kwa miaka kadhaa sasa na kila mwaka tumekuwa tukionyesha staili tofauti katika uboreshaji wa Tuzo hizi, na mwaka huu tumezidi kuboresha zaidi ili kuwa katika levo ya kimataifa zaidi na wale watakaobahatika kufika katika onyesho hili watakuwa mashahidi,” alisema Minja
“Lengo la Tuzo hizi ni kufikisha muziki wa Tanzania katika kilele cha mafanikio, pamoja na kuwapa nafasi kubwa wasanii wa hapa nyumbani kutoa burudani kama sehemu ya kuonyesha vipaji vyao katika sanaa ya muziki,” alisema Minja.
Pia alitaja viingilio vya onyesho hilo kuwa ni Sh. 25,000 kwa VIP na Sh. 15,000 kwa viti vya kawaida na tayari tiketi zimeanza kuuzwa katika vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Masoko wa Kampuni ya Bia TBL, David Minja (wapili kushoto) akimkabidhi Tunzo za Kilimanjaro Music Awards 2011, Mratibu wa Tunzo hizo kutoka Baraza la Sanaa la Taifa BASATA, Angelo Luhala, ikiwa ni sehemu ya kukamilika kwa maandalizi ya onyesho la kuwatunuku Tuzo wasanii la Kili Music Awards 2011, linalotarajia kufanyika Machi 26 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini. Kushoto ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe (kulia) ni Ofisa Uhusiano wa TBL, Doris Malulu.
Viongozi hao wakisimama kwa dakika moja kuomboleza msiba wa wasanii wa Kundi la 5 Star, waliofariki kwa ajali ya gari jana huko maeneo ya Mikumi.
Viongozi hao wakisimama kwa dakika moja kuomboleza msiba wa wasanii wa Kundi la 5 Star, waliofariki kwa ajali ya gari jana huko maeneo ya Mikumi.
No comments:
Post a Comment