VIONGOZI wawili wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), wanatarajiwa kuondoka Dar es Salaam kesho Jumatatu, Machi 21, 2011 kuelekea Seoul, Korea Kusini kuhudhuria Mkuu wa AIPS.
Mkutano huo wa 74 wa Chama cha Kimataifa cha Waandishi wa Habari za Michezo (AIPS) utaanza Jumanne Machi 22 hadi Machi 27, mwaka huu huko huko Korea, Kusini.
TASWA katika mkutano huo itawakilishwa na Makamu Mwenyekiti Maulid Kitenge na Katibu Mkuu Msaidizi, George John ambao wataondoka kesho alasiri kwa ndege ya Shirika la Ndege la Qatar.
TASWA inaamini mkutano huo utakuwa na manufaa kwa chama pamoja na waandishi wa habari za michezo kwa ujumla hapa nchini kutokana na mada mbalimbali zitakazojadiliwa.
Pia Taswa inawashukuru wote waliofanikisha safari hiyo ambao ni Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) waliosaidia tiketi za wahusika kwenda Korea Kusini na kurudi Dar es Salaam.
Tunaamini msaada mkubwa wa NSSF na TFF ni ishara ya ushirikiano mzuri uliojengwa baina ya TASWA na taasisi hizo mbili.
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
20/03/2011
No comments:
Post a Comment