Habari za Punde

*WAFANYAKAZI WA BARRICK WAJITOLEA DAMU KUWASAIDIA WAATHIRIKA WA MABOMU

Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Barrick, Teweli Teweli, akijitolea damu na Fundi Sanifu wa Maabala ya Damu Salama, kutoka Wizara ya Afya, Elizabeth Mgaya, wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo pamoja na makampuni jirani walipokusanyika kutoa damu kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mabomu wa Gongolamboto. Zoezi hilo la utoaji damu lilifanyika leo mchana kwenye ofisi za Barrick zilizopo Masaki jijini Dar es Salaam.
Elizabeth (kulia) akimpima damu Teweli, kabla ya kuanza zoezi la kumtoa damu.
Mtaalam wa utoaji damu salama kutoka Wizara ya Afya, Peter Chami, akimtoa damu, Mfanyakazi wa Barrick, Sundy Malomi, wakati wa zoezi hilo.
Sundy, akijifunika khanga akiogopa kuangalia damu yake wakati ikitoka kuingia katika kifaa cha kukingia damu hiyo, anasema kuwa leo hii ni mara yake ya kwanza kutoa damu tangu azaliwe. Kushoto ni wafanyakazi wa makampuni jirani na Barrick, wakisubiri kutoa damu.




No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.