Habari za Punde

*WALEMAVU WA NGOZI WAKABIDHIWA MSAADA WA MAFUTA YA KUZUIA MIONZI

Mratibu wa Programu kutoka Hands of Africa Foundation, Joseph Magutu (kulia) akikabidhi msaada wa mafuta ya kuzuia mionzi ya jua kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) kwa Stamili John, mkazi wa Kongwa mkoani Dodoma ambaye amelazwa katika Hospitali ya Ocean Road iliyopo jijini Dar es Salaam kwa ajilia ya tatizo la kansa ya ngozi.
Msaada huo ambao ni mafuta ya watoto na watu wazima wenye thamani ya shilingi milioni 8.2, umetolewa na shirika rafiki la Society for Threatened People la nchini Ujerumani utapelekwa kwa Albino wa mkoa wa Kilimanjaro pamoja na mikoa mingine jirani na wagonjwa wa saratani wenye ulemavu wa ngozi walioko katika Hospitali ya Ocen Road. Picha na Anna Nkinda - Maelezo
Stamili John (kushoto) mkazi wa Kongwa mkoani Dodoma ambaye amelazwa katika Hospitali ya Ocean Road iliyopo jijini Dar es Salaam akimshukuru Mratibu wa Programu kutoka Hands of Africa Foundation Joseph Magutu (kulia) mara baada ya kumkabidhi msaada wa mafuta ya kuzuia mionzi ya jua kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino).

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.