Habari za Punde

*BENDI YA MASHUJAA YAFUNIKA ONYESHO LA UTAMBULISHO WA WAPYA

Kiongozi na mwimbaji wa bendi ya Mashujaa Musica, Jado Fidiforce (kushoto) akimtambulisha rapa mpya aliyejiunga na bendi hiyo akitokea bendi ya Diamond Musica, Sauti ya Radi, wakati wa onyesho la utambulisho wa wanamuziki wapya waliojiunga na bendi hiyo, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Kijiji cha Makumbusho juzi. Mpiga Tumba wa Mashujaa, Dullah Ngoma, akiwapagawisha mashabiki wake kwa midundo ya tumba wakati wa onyesho hilo.
Mwimbaji wa bendi ya Mashujaa Musica, Jado Fidiforce, akionyesha umahiri wake wa kucheza miondoko ya bendi hiyo.
Wanenguaji wa kiume wa Mashujaa, Kelvin Ulaka na Maga One Star, wakipozi kwa picha.
Jado (katikati) akiwaongoza wenzake kushambulia jukwaa wakiimba vibao vya bendi hiyo.
Wanenguaji wa kike wa bendi hiyo, wakipozi kwa picha. Kutoka (kushoto) ni Rose Twiga, Salma Teketeke, Mariam Lelape, Pendo Bonzo, Queen Nasra na Corando Bikolakoza.
Mashabiki waliohudhulia onyesho hilo, wakisakata sebene.
Rapa na mwimbaji wa bendi ya Mapacha Watatu, Khalid Chokoraa (katikati) akishambulia jukwaa na wanenguaji wake wakati wa onyesho lao la kusindikiza bendi ya Mashujaa Musica iliyokuwa ikitambulisha wanamuziki wapya waliojiunga na bendi ya Mashujaa, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Kijiji cha Makumbusho. Kulia ni Mariam Bercy (kushoto) ni Sabrina Pazi ‘Loketo.
Kalala Junior, akiigiza rap yao mpya ya Kikombe cha Babu, kuwanywesha kikombe cha dawa wanamuziki wake kama Babu wa Loliondo.
Mpiga tumba wa Mapacha watatu, akishambulia.
Kalala Junior, akipagawishwa na sahabiki wa Mapacha Watatu, aliyepanda jukwaani na kuanza kusakata sebene la bendi hiyo.
Mashabiki waliojitokeza wakiwa tuli katika meza zao kushuhudia kinachoendelea jukwaani. Kulia ni mmoja wa waigizaji mahiri wa Tasnia ya Filam.






No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.