Habari za Punde

*SHEREHE ZA MIAKA 47 YA MUUNGANO ZANZIBAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akikagua gwaride wakati wa Sherehe za maadhimisho ya miaka 47 ya Muungano zilizofanyika kwenye Uwanja wa Amani mjini Zanzibar leo mchana.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Kikwete, akipunga mkono kuwasalimia w3ananchi na wageni wakati alipokuwa akiingia kwenye Uwanja wa Amani katika sherehe za maadhimisho ya miaka 47 ya Muungano mjini Zanzibara.


Askari wa Jeshi la Wananchi wakiloa na mvua bila kujali wakati wakiwa kwenye shughuli za ulinzi katika sherehe hizo. Mvua hiyo ilianza kunyesha na kuzua kizaa zaa mahala hapo wakati ratiba ya shughuli hiyo ikielekea ukingoni na kusababisha baadhi ya mambo yaliyokuwa katika ratiba hiyo kuahirishwa.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi, James Mbatia, wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu mjini Zanzibar leo mchana baada ya kumalizika kwa sherehe za maadhimisho ya miaka 47 ya Muungano.

Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi Zakia Bilal, akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Ibrahim Lipumba, wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu Zanziba, baada ya kumalizika kwa sherehe za maadhimisho ya miaka 47 ya Muungano mjini Zanznibar.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Kimataifa ya Hazina ya Jijini Dar es Salaam, wakionyesha umahiri wao wa kucheza Sarakasi wakati wa Sherehe za maadhimisho ya miaka 47 ya Muungano zilizofanyika kwenye Uwanja wa Amani mjini Zanzibar.

Sehemu ya washereheshaji wa sherehe hizo wakiwa jukwaani wakichora mfano wa Bendera ya Tanzania. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal (katikati) Rais wa Zanzibar, Dkt.Ali Mohamed Shein (kulia) na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, wakiwa jukwaani wakati wa sherehe hizo.


Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi Asha Bilal na Waziri Mstaafu, Edward Lowasa, wakiwa jukwaani wakiimba wimbo wa Taifa, wakati wa wa sherehe za maadhimisho ya sherehe za miaka 47 ya Muungano zilizofanyika kwenye Uwanja wa Amani mjini Zanzibar.

Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi Zakia Bilal na viongozi wengine wa Kiserikali, wakiwa jukwaani wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 47 ya Muungano zilizofanyika kwenye Uwanja wa Amani mjini Zanzibar.


Askari Polisi wa Kike wakipita mbele ya Jukwaa Kuu.


Askari wa kutuliza ghasia FFU, wakipita mbele ya Jukwaa Kuu na kutoa heshima kwa mgeni rasmi wakati wa sherehe hizo.

Baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya na nyimbo za Injili Dokey na Frola Mbasha, waliohudhulia sherehe hizo kwenye Uwanja wa Amani mjini Zanzibar.

Chege, Tundaman na wenzao wakiwa ni miongoni mwa waliohudhulia sherehe hizo.

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Ibrahim Lipumba, akiwa ni miongoni mwa wageni waalikwa waliohudhulia sherehe za maadhimisho ya miaka 47 ya Muungano, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Amani mjini Zanzibar.






























No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.