Shirika la Oikocredit
kujiletea maendeleo katika jamii zao.
350/-, Musoma Sacco milioni 200/- na ile ya Shinyanga Foundation Fund shilingi milioni 150/-
Akikabidhi msaada huo Meneja wa Oikocredit Tanzania Deus Manyenye amesema kuwa taasisi nyingi za kifedha haziamini kusaidia kwenye miradi ya watu masikini hivyo shirika
“Oikocredit hupendelea mno miradi ambayo wanawake wanajumuishwa kwenye ngazi za maamuzi. Sisi tunaamini kwamba watu
masikini wanaweza kujijengea maisha mazuri wakipewa fursa
Akifafanua Meneja huyo amesema, tangu Oikocredit ianzishwe nchini mwaka 2006 tayari wameshakopesha miradi 30 yenye thamani ya shilingi bilioni 30 ili kuwasaidia watu masikini na wasiojiweza wanaoishi mijini na vijijini.
Takwimu zilizotolewa na shirika
Akizungumza kwa niaba ya wenyeviti wa Saccos zilizokopeshwa fedha hizo, Mwenyekiti wa Shinyanga Foundation Fund, Paulo Sangija alisema watatumia fedha hizo kwa wakati ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa ya kuikomboa jamii kuondokana na umasikini.
“Mkopo huu umefungua mlango wa pili, tutakachohakikisha sisi ni jamii inanufaika na fedha hizi kwani tukizifuja tutadidimia zaidi. Ukikosa uwezo vilevile mbinu za upatikanaji wa mikopo unakosekana, tunashukuru na hatutakuangusha,” alisema Sangija.
Mbali na hayo Oikocredit ilishazikopesha jumla ya shilingi bilioni 2.1/- kwa YWCA Moshi na Saccos ya Wazalendo ili zitumike kuiwezesha jamii ya watu wa kipato cha chini. Fedha zilizotolewa zilitumika kwa ajili ya ukarabati wa jengo la makao makuu ya YWCA Moshi na uwezeshaji jamii ili ijiendeleze kimaisha kupitia Wazalendo.
Mwenyekiti wa Shinyanga Foundation Fund, Paulo Sangija, akisisitiza jambo wakati wa hafla ya kukabidhiwa hundi zenye jumla ya shilingi milioni 700/- kwa Saccos za Mwanza, Musoma na Shinyanga Foundation Fund iliyofanyika jijini Mwanza hivi karibuni. Katikati ni Meneja wa Oikocredit
Meneja wa Oikocredit
No comments:
Post a Comment