Mratibu wa Tamasha la michezo ya Jumuiya ya Mabohora, 'Annadil Burhan East African Sports Festival ', Taher Kitisa, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Tamasha hilo lenye lengo ya kusherehekea kutimiza miaka 100 kwa kiongozi wao Dr. Syedna Mohammed Burhanudin Sayeb (TUS), ambapo tamasha hilo litafikia kilele chake siku ya jumatatu kwa kuadhimisha na paredi ikiwa ni pamoja na kutoa zawadi kwa washindi walioshiriki katika michezo mbalimbali ya Snooker, mpira wa miguu, Tenes, Table Tenes, Clicket, Swimming na Darts,tamasha hilo limeshirikisha timu za jumuiya za Mabohora kuto Nairobi, Tanga, Malindi, Morogoro, Arusha na Dar es Salaam.
Hata hivyo mchezo wa Clicket katika tamasha hilo uliingia dosari baada ya kunyesha mvua kubwa wakati mchezo huo ukiendelea na kusababisha kuahirishwa. Hapa ni wahudumu wa uwanja huo wa Annadil Burhan, wakifunika uwanja huo ili usiharibike.
No comments:
Post a Comment