Mkurugenzi Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (wapili kushoto), akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadick, moja ya vifaa vinavyotumika kumuhudumia mzazi wakati wa kujifungua wakati wa hafla fupi ya kukabidhi jengo la uzazi la Zahanati ya Kivule, lililokarabatiwa na kampuni hiyo baada ya kulipuliwa na mabomu yaliyolipuka katika Kikosi cha Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) cha Gongo la Mboto cha KJ 511, Dar es Salaam Februali 16, mwaka huu. TBL imetumia sh milioni 30 kukarabati na kununua vifaa vilivyoharibiwa. Kulia ni Mhandisi wa Ujenzi wa TBL, John Malisa (kushoto) ni Doris Malulu ambaye ni Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo.
Afrika yatakiwa kuongeza wanahabari mahiri wa sayansi kuchochea ubunifu na
maendeleo
-
*Na Veronica Mrema, Pretoria*
*Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu wa Afrika Kusini, Profesa Blade
Nzimande, amesema Bara la Afrika linahitaji kwa...
24 minutes ago
No comments:
Post a Comment